Home Habari za Simba Leo SIMBA KUACHANA NA KIPA WAO…SABABU NI HIZI

SIMBA KUACHANA NA KIPA WAO…SABABU NI HIZI

Habari za Simba

MABINGWA wa Ligi ya Wanawake SIMBA Queens msimu ujao haitaendelea na kipa wa timu hiyo, Zubeda Mgunda baada ya kumaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu.

Kipa huyo alisajiliwa na Simba mwaka 2018 akidumu kikosini hapo kwa takribani misimu sita na kuiwezesha timu hiyo kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) mara nne.

Inaelezwa sababu ya kuondolewa kikosini hapo ni kutokana na kushindwa kupata namba mbele ya kipa namba moja, Mkenya Carolyne Rufaa.

Ujio wa Rufaa Simba mwaka 2022 umekuwa ukimpa wakati mgumu wa kupata namba Mgunda ambaye msimu uliopita hakucheza mchezo hata mmoja wa Ligi.

Mmoja wa viongozi wa Simba (jina tunalo) amesema kuwa klabu hiyo itaachana na wachezaji sita ikiwemo kipa ili kupisha nafasi ya wachezaji wengine.

“Sio Mgunda tu wapo karibu sita kocha amebainisha kuwa hana mpango nao hivyo tumeachana naye na tumeamua tubaki na makipa wawili, Carolyne na Gelwa Yona,” amesema kiongozi huyo.

“Mgunda ni kipa mzuri nafikiri miaka ya 2021 watu walimuona uwezo wake lakini ameshindwa kuendeleza kiwango chake hivyo tutaachana naye.”

Timu hiyo imeendelea kujiimarisha zaidi kwaajili ya msimu ujao,  ikumbukwe Simba Queens ndiye Mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake hivyomsimu ujao watachez michuano ya Kimataifa.

Mara ya mwisho   kucheza michuano hiyo, Simba ilifikia hadi hatua ya Nusu Fainali na kuondoshwa wakiwa wameweka rekodi ambayo hadi sasa haijavunjwa.

Ikumbukwe msimu uliopita timu ya Wanawake ya JKT Tanzania nayo ilishiriki michuano hiyo lakini hawakufika hata hatua ya Nusu Fainali wakaondolewa.

SOMA NA HII  SIMBA YAWAONGEZA MKATABA MZAMIRU & ISRAH...MWINGINE ATAMBULISHWA