Home Habari za michezo UZI MPYA WA SIMBA MSIMU HUU 2024/25 HUU HAPA….

UZI MPYA WA SIMBA MSIMU HUU 2024/25 HUU HAPA….

Jezi Mpya za Simba 2024

Mabingwa wa Zamani wa Tanzania Simba SC mchana wa leo hii wamezindua jezi mpya kwa ajili ya msimu ujao wa ligi , msimu wa 2024/25 .

Hizi ndio jezi mpya za Simba SC kuelekea msimu wa 2024/2025 ambazo zimetambulishwa katika Hifadhi ya Taifa ya Mikuni.

Simba SC wametambulisha jezi za aina tatu nyumbani nyekundu, ugenini nyeupe na blue ni jezi mbadala (Third Kit).

KIBU ATAJWA.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa hakuna usajili ambao uliwatetesa viongozi hao kama ule wa kiungo mshambuliaji wao, Kibu Denis.

Kauli hiyo ya Ahmed imekuja ikiwa ni siku chache baada ya mchezaji huyo kugoma kujiunga na kambi ya klabu huko Misri na kutimkia nchini Norway ambako anadaiwa kupata dili.

“Hakuna usajili uliotutesa Simba kama wa kumuongezea mkataba Kibu Denis. Alikuwa anasema ntaongeza mkataba, ntaongeza mkataba Anapitia huku anatokea huku. Wavimba macho nao walikuwa wanamvizia Hatukulala wiki mbili.

“Watu wanasema ana goli moja. Ndio ana goli moja lakini anajituma sana. Kibu ni aina ya wachezaji ambao wanacheza kama timu za baba zao, Hakuna timu inatamani kukutana na Kibu,” amesema Ahmed Ally.

SOMA NA HII  PAMOJA NA IHEFU KUWASAIDIA JUZI...SIMBA WAENDELEA KUWEWESEKA NA YANGA...