Habari za michezo

SIMBA WAINGIA MAKUBALIANO HAYA NA TP MAZEMBE

Staff Desk November 16, 2023 6:44 am

Mmiliki wa Klabu ya TP Mazembe, Moise Katumbi amesema tumeingia makubaliano na Klabu ya Simba ili kushirikiana katika mambo mbalimbali yanayohusu mpira.

Katumbi amesema makubaliano ambayo wanayo na Simba ni katika utawala, uchumi na kuuziana wachezaji.

Ikumbukwe kuwa msimu uliopita Simba waliofanya biashara na TP Mazembe ya kuuziana mchezaji Jean Baleke ambaye ameleta chachu kubwa katika mpira wetu kutokana na uwezo wake wa kufumania nyavu

Moise ameishukuru Simba kwa mapokezi yao toka wamefika hapa nchini ambayo watakuwa na mchezo wa (AFL) dhidi ya Es Tunis ya Tunisia.

KIBOKO YENU ANAKUJA HUENDA YANGA IKAWA NDIO TIMU YA KWANZA KWENYE REKODI HII BONGO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply