Home Habari za Yanga Leo ANDABWILE NI MALI YA YANGA…YANGA YAIJIBU SIMBA

ANDABWILE NI MALI YA YANGA…YANGA YAIJIBU SIMBA

Habari za Yanga, Aziz Andabwile

KLABU ya Yanga imekamilisha usajili wa kiungo mkabaji, Aziz Andabwile kutoka Singida Fountain Gates kwa mkataba wa miaka miwili.

Kiungo huyo amejiunga na Yanga kuongeza nguvu eneo la kiungo cha ukabaji ambapo anaungana na Khalid Aucho na Jonas Mkude.

Usajili wa kiungo huyo unamaanisha kwamba anakwenda kuchukua nafasi ya Zawadi Mauya ambaye hivi karibuni aliondoka baada ya mkataba wake kumalizika akiwa ameitumikia timu hiyo kwa miaka minne kuanzia 2020 hadi 2024.

HABARI ILIJUKANA KITAMBO

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Singida Fountain Gate kilisema kuwa ni kweli kuna mazungumzo kati yao na Yanga kwa ajili ya kiungo huyo. “Yanga wametuma ofa na mazungumzo baina yetu na wao yanaendelea, yapo kwenye hatua nzuri na muda wowote mambo yakienda sawa atatambulishwa kama mchezaji wao,” kilisema chanzo hicho.

“Tupo Dar es Salaam sambamba na mchezaji kwa ajili ya kukamilisha dili hilo. Uwezekano ni mkubwa wa kumuuza kuliko kubaki Singida Fountain Gate hivyo mtarajie lolote.” Wakati huohuo, Yanga imekiri kuwa na uhitaji wa kiungo mkabaji ambaye atasaidiana na Khalid Aucho ukiondoa Jonas Mkude ambaye pia anatakiwa kuwa na mshindani wake.

“Kati ya sehemu ambazo tunahitaji kuboresha kwa ajili ya msimu ujao ipo nafasi ya kiungo mkabaji. Ndiyo maana wamekuwa wakitajwa wachezaji wengi wanaocheza eneo hilo. Mambo yakiwa tayari kila mmoja atafahamu ni kiungo gani anasajiliwa,” kilisema chanzo kutoka Yanga.

“Ukiangalia ndani ya Yanga ukimuondoa Aucho, kuna Jonas Mkude, tulikuwa na Zawadi Mauya ambaye tayari ameondoka kikosini baada ya mkataba wake kumalizika, hivyo benchi la ufundi limeona kuna haja ya kitu kifanyike kulingana na matakwa yao.”

Andambwile anakuwa mchezaji wa tano mpya kutambulishwa ndani ya Yanga kipindi hiki cha usajili wa dirisha kubwa baada ya Clatous Chama, Prince Dube, Chadrack Boka na Khomeiny Aboubakar.

SOMA NA HII  BREAKING NEWS...SIMBA YAMUACHA SAIDOO...SABABU ZATAJWA.