Home Habari za Simba Leo BREAKING NEWS…SIMBA YAMUACHA SAIDOO…SABABU ZATAJWA.

BREAKING NEWS…SIMBA YAMUACHA SAIDOO…SABABU ZATAJWA.

HABARI ZA SIMBA

UONGOZI WA SIMBA, umefikia makubaliano ya kuachana na mchezaji wao Raia wa Burundi Saidoo Ntibazonkiza ambaye alijiunga na klabu hiyo kwa miaka miwili.

Mkataba wa Saidoo Ntibazonkiza ulimalazika mwaka huu, hku akiwagawa viongozi wa timu hiyo, wapo waliotaka wamuongeze Mkataba na wengine walitaka apewe Thank You.

Hatimaye upande wa waliotaka mchezaji huyo kuachwa wameshinda, na mida ya mchana wa Saa 7 Juni 18, Taarifa ya Simba ilieleza kuachana na mfungaji bora wao kwa miaka miwili, msimu uliopit alikuwa na mabao 17, huku msimu huu akifunga mabao 11.

Moja ya sababu iliyopelekea Saidoo kuachwa na Simba, ni suala la umri mkubwa, mchezaji huyo ana miaka 37 suala ambalo linamfanya kushindwa kuhimili kukimbizana kwa kasi kubwa uwanjani.

Mgunda amesema kuwa suala la wachezaji kutajwa kuwa na umri mkubwa halina uhusiano na matokeo uwanjani kwa kuwa kila mmoja anafanya kazi yake kwa mujibu wa maelekezo ambayo yanatolewa na benchi la ufundi.

“Kuhusu umri kutajwa kuwa sababu hilo haliwezi kuwa kweli kwa kuwa kila mchezaji anacheza kwa mujibu wa maelekezo ya benchi la ufundi hivyo kinachotokea ni kile kinachofanyika uwanja wa mazoezi.

“Wachezaji wapo vizuri na wanafanya kazi kubwa kutimiza majukumu yao ndani ya uwanja tuna amini kwamba itakuwa hivyo, mashabiki wazidi kuwapamoja nasi tutakuwa imara.”

Saidoo pia amewahi kucheza YANGA SC kabla ya  kutua Simba.

SOMA NA HII  HAJI MANARA KUHUSU KUMSHAURI FEISAL KUCHEZEA SIMBA NA SIO YANGA