Home Uncategorized TAIFA STARS YAMWEKA NJIA PANDA TANASHA

TAIFA STARS YAMWEKA NJIA PANDA TANASHA


Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imemuweka njia panda mrembo wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna Oketch ashindwe kujua asimame upande gani kati ya Taifa Stars na timu ya nchini kwao, Harambee Stars.

Kwa mujibu wa chambuzi mbalimbali zilizofanywa na mitandao tofauti ya nchini Kenya, presha ya Tanasha itakuwa juu kabla na hata baada ya mechi iliyochezwa usiku wa kuamkia jana na kuzikutanisha timu hizo mbili ambapo Kenya waliibuka na ushindi wa bao 3-2

“Yaani kwa kweli Stars inamuweka mtegoni Tanasha maana anapaswa kumsapoti mpenzi wake na wakati huohuo Harambee ni timu ya kwao.

“Bahati mbaya sana mechi hiyo ndiyo inatoa picha ya nani ana matumaini ya kusonga mbele, kwa vyovyote vile Tanasha hakuwa na ujasiri wa kuufurahia sana ushindi wa Harambee,” ulichambua mmoja wa mitandao hiyo.

Hata hivyo, licha ya maoni hayo kutikisa sana kwenye mitandao ya kijamii, mwanzoni Tanasha alionekana kuwa kimya lakini siku ya game akaibukia mitandaoni na kuisapoti harambe Stars lakini upande wake wakati Diamond mara kadhaa ameonekana kujipambanua kwa kuiunga mkono Taifa Stars.

Taifa Stars na Harambee Stars wanashiriki michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) inayoendelea nchini Misri ambapo mataifa hayo mawili yapo katika moja la Kundi C. Katika kundi hilo, Senegal walichezea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Algeria.

SOMA NA HII  MUUAJI WA AL RABITA FURAHA YAKE IPO HAPA