Home Habari za Yanga Leo BAADA YA KUSAJILIWA NA YANGA PRINCE DUBE AFUNGUKA…NAFURAHI KUWA YANGA.

BAADA YA KUSAJILIWA NA YANGA PRINCE DUBE AFUNGUKA…NAFURAHI KUWA YANGA.

Habari za Yanga-Prince Dube.

Mshambuliaji wa Yanga SC, Prince Dube amesema kuwa anafurahia kusajiliwa na Klabu hiyo kwani ilikuwa ndoto yake ya muda mrefu kucheza soka kwenye klabu kubwa kama Yanga.

Dube amesema hayo leo wakati akiondoka na Kikosi cha Yanga kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya michuano ya Toyota Cup na michezo mingine ya kirafiki ambayo wamealikwa na kaizer Chiefs.

“Nafurahi kucheza Yanga, nafurahi kucheza na Chama na Aziz Ki, kuna wachezaji wakubwa hapa na kila mchezaji anatamani kucheza Yanga ili ushinde makombe. Ilikuwa ndoto yangu kucheza timu kubwa na nipo hapa kwa ajili ya kufanya kazi.

“Nimepitia kipindi kigumu na sasa natamani kufurahi na kuitumika klabu yangu ya sasa. Mambo yanakwenda vizuri, nimekaribishwa vizuri kuanzia kwa mashabiki, viongozi, na benchi la ufundi na kila mtu na najisikia furaha.

“Nipo hapa kuongeza nguvu kwenye timu yetu ya Yanga ili tuweze kushinda makombe. Ni timu yenye mashabiki wengi wamenionesha upendo na makaribisho makubwa, siku ya Wananchi waje kushuhudia mambo makubwa. Mimi nipo tayari kuwafurahisha na kama nitakuwa timamu kimwili kwenye kila mchezo,” amesema Prince Dube.

Prince Dube amejiunga na Yanga kama mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake na waajiri wake wa zamani Azam FC.

Baada ya kufanya hivyo klabu ya Azam FC ilimtaka mchezaji huyo kulipa fidia ya mkataba wake baada ya hukumu kutoka Kamati ya Usuluhishi ya TFF.

Prince Dube aliilipa klabu hiyo malipo yote na kuwa huru, ndipo alipofanikiwa kusajiliwa na Yanga na hadi sasa amesafiri na timu hadi Afrika Kusini kucheza mechi ya kwanza ya Kimataifa ya Kirafiki dhidi ya FC Augsburg akiwa na uzi wa Yanga.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA USAJILI YANGA...HERSI AWEKA MAMBO HADHARANI...AFUNGUKA HAYA JUU YA VIFAA VIPYA...