Home Uncategorized LYANGA AJIFUNGA MIAKA MIWILI AZAM FC

LYANGA AJIFUNGA MIAKA MIWILI AZAM FC


AYOUB Lyanga, kiungo mshambuliaji mwenye mabao nane na pasi nane alipokuwa ndani ya Coastal Union leo Agosti 2 amesaini kandarasi ya miaka miwili kuitumikia timu hiyo.

Lyanga amefanyiwa vipimo mapema leo na kuonekana yupo fiti jambo ambalo limewafanya Azam FC wampe dili la miaka miwili.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wamekamilisha usajili kwa mapendekezo ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba.

“Tumekamilisha usajili wa Lyanga kwa mkataba wa miaka miwili, bado kazi imeanza kwani huyu ni nyota wa tatu kwetu kutambulishwa.

“Hesabu zetu ni kuona kwama timu inakuwa imara zaidi na kuleta ushindani kwa msimu ujao, kikubwa mashabiki waendelee kutupa sapoti,” amesema.

SOMA NA HII  SIMBA YAFUNGUKIA ISHU YA MKUDE KUFUKUZWA SIMBA