Home Habari za Simba Leo BAADA YA KUWAONA YANGA…FADLU DAVIDS ABADILI MIFUMO SIMBA.

BAADA YA KUWAONA YANGA…FADLU DAVIDS ABADILI MIFUMO SIMBA.

habari za simba- Fadlu Davids

FADLU Davids Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kazi kubwa iliyopo kwa sasa ni kuwaandaa wachezaji kuwa tayari kwa ushindi kwenye mechi zao za ushindani zijazo huku mechi yao ya kwanza ya ushindani ni dhidi ya mtani wao Yanga itakayopigwa Agosti 8.

Kuelekea msimu wa 2024/25 Simba imeweka kambi Misri ikiwa na wachezaji kama Mzamiru Yassin, Zimbwe, Ally Salim na ligi inatarajiwa kuanza Agosti 16 2024 huku mabingwa wakiwa ni Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Simba ni wawakilishi wa Tanzania kwenye anga la kimataifa ambapo ni katika Kombe la Shirikisho Afrika huku zipo timu mbili kutoka Tanzania nyingine ni Coastal Union.

Fadlu amebainisha kuwa mazoezi ambayo yanafanyika ni maalumu kwa kuwa na kikosi cha ushindi kitakachowapa matokeo chanya katika mechi za msimu wa 2024/25.

“Kikubwa ni kuona kwamba tunawapa mbinu za kutafuta ushindi uwanjani hili litaongeza uwezo wao zaidi na kuwa wapambanaji kwenye mechi za ushindani ambazo tutacheza.

“Mashabiki wanahitaji kuona matokeo yakipatikana hivyo ni muhimu kuwa pamoja nasi kwenye mechi zote na wachezaji wanatambua kwamba jambo la msingi ni kufanya vizuri.”

Simba ipo Misri katika Mji wa Ismailia ikijifua kwaajili ya msimu mpya wa 2024/25 ikiwa na nyota wapya kama vile Joshua Mutale, Steve Mukwala, Chamou Karaboue, Valentino Nouma, Valentine Mashaka, Yusuph Kagoma, Augustine Okejepha, Jean Charles Ahoua, Abdulrazk Hamza, Kelvin Kijili, Awesu Awesu huku usajili wa Lameck Lawi sakata lake lipo TFF.

Mchezo wa kwanza wa Simba utachezwa katika Simba Day, timu tutakutajia Taarifa ikitoka, lakini huenda zamu ya kulipa kisasi kwa Yanga ikawa Agosti 8, kwenye mechi ya Nusu Fainali Ngao ya Jamii.

SOMA NA HII  SIMBA TUMBO JOTO MECHI YAO DHIDI YA MTIBWA SUGAR.... ISHU IKO HIVI