Home Uncategorized SIMBA YAIFAUATA POLISI TANZANIA, MOSHI KUMALIZA NGWE YA MWISHO

SIMBA YAIFAUATA POLISI TANZANIA, MOSHI KUMALIZA NGWE YA MWISHO

TIMU ya Simba leo Julai 24 imeifuata Polisi Tanzania ya Moshi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara  utakaopigwa Julai 26.

Seleman Matola ambaye ni Kocha Msaidizi wa kikosi hicho alikinoa kikosi hicho kabla ya kuibukia Simba.

Mchezo wa Kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa, Simba ilishinda mabao 2-1.

Bao la ushindi lilifungwa na Ibrahim Ajibu dakika za lala salama na kuipa pointi tatu Simba.

Timu zote mbili zina uhakika wa kubaki ndani ya Ligi, Simba ni Mabingwa wana pointi 85 wakiwa nafasi ya Kwanza na Polisi Tanzania ipo nafasi ya 5 na pointi 55 zote zimecheza mechi 37.

SOMA NA HII  SIMBA: HAKUNA UADUI DHIDI YA YANGA