Home Habari za Yanga Leo FRIJI LA BALEKE HALIGANDISHI…AJITAMBULISHA YANGA

FRIJI LA BALEKE HALIGANDISHI…AJITAMBULISHA YANGA

Habari za Yanga-Baleke

Mshambuliaji wa TP Mazembe, Jean Baleke ambaye alikuwa kwa mkopo kunako klabu ya Al Ittihad ya Libya amethibitisha kujiunga na Young Africans Sc kama mchezaji mpya klabuni hapo kwa msimu ujao wa 2024/25.

Kupitia Insta Story yake Baleke ameposti picha akiwa ndani ya uzi wa Yanga Sc ikiwa ni Taarifa ya moja ya chombo cha habari kilichothibitisha ujio wake Jangwani.

Nyota huyo anatarajiwa kutangazwa hivi karibuni na klabu hiyo baada ya kusitisha mkataba wake wa mkopo na miamba hiyo ya Libya na kujiunga na Wananchi.

Mshambuliaji huyo wa ambaye amewahi kuitumikia Simba Sc, amejiunga na kambi ya mazoezi ya Wananchi licha ya kimya kingi juu ya utambulisho wake kama mchezaji mpya klabuni hapo.

Baleke ameripotiwa kujiunga na Mabingwa hao wa nchi kwa mkopo wa msimu mzima na anatarajiwa kutangazwa muda mfupi ujao kama mchezaji mpya klabuni hapo.

Klabu ya Yanga imesajili wachezaji kibao wenye majina mkubwa na uwezo uwanjani,  kuna Clatous Chama, Prince Dube, Chadrack Boka, Aziz Andabwile, na sasa Duke Abuya.

Wachezaji wanaohusishwa zaidi kujiunga na Simba, ni Jean BALEKE aliyewahi kucheza Simba kwa msimu mmoja na nusu akifunga jumla  ya mabao 16, kisha akatimkia kwenda klabu ya Al Ittihad ya Libya.

Akiwa huko Libya alifanikiwa kuwa mfungaji bora huku akifunga hat trick 3.

SOMA NA HII  SIMBA NDIO MTAIJUA LEO...WAARABU WAINGIA UBARIDI TAYARI