Home Habari za Simba Leo ISHU YA MANULA KWENDA AZAM FC..IKO HIVI

ISHU YA MANULA KWENDA AZAM FC..IKO HIVI

Habari za Simba SC

ZA NDAANI Kutoka Simba ni kwamba, Mchezaji Aishi Manula amebakisha mkataba wa mwaka mmoja na Simba SC, Lakini yeyé yupo tayari kuondoka klabuni kwenye dirisha hili kubwa.

Chanzo cha kuaminika kimesema Aishi Manula haoni hadhi yake kama inaheshimiwa Simba SC na badala yake kuchafuliwa kwa mambo ambayo hayampendezi.

Azam FC wameiandikia barua Simba SC kumtaka Aishi Manula aende huko kwa mkopo wa Msimu mzima, jambo ambalo Aishi ameridhia kwa kuwa ukiisha atakuwa free agent.

Baadhi ya Viongozi wa Simba SC wanataka asalie wakidai bado ni kipa Mzuri sana ila anapitia ugumu tu, Hivyo asalie apiganie namba yake kwa kuwa Wapo ambao hawaamini Ayoub Lakred kama anatosha ila anapitia form Nzuri tu kwa Sasa.

Wengine wanasema inatosha kutokana na kiwango chake koporomoka tokea atoke kuuguza majeraha yake.

Lakini hadi sasa Barua ya Azam FC bado haijajibiwa na Simba SC, Viongozi wa Simba wameamua kupiga kimya wakati wakitafakari kwa kina kabla ya kufanya maamuzi.

Mara ya mwisho Manula kucheza Simba alikula goli 5 kutoka Yanga, ambapo kumekuwa na uvumi kwamba mechi hiyo mchezaji huyo ni moja ya watu waliohujumu timu.

Kwa taarifa za ndani Simba, kocha wa Magolikipa wa timu hiyo Dani Cadena alisem kwamba yeye binafsi hakuridhia Manula adake, kwa sababu alitoka kwenye majeraaha hivyo hakuwa fiti lakini Kocha Robertinho alilazimisha mchezaji huyo kudaka.

“Siku mbili kabla ya mechi, katika kikao na viongozi wa bodi hakuna hata mmoja aliyeniuliza kuhusu hali ya utimamu wa mwili wa Aishi Manula, lakini Robertinho alisema Aishi Manula yuko fiti atacheza”

“Baadae nilienda kuongea na Manula nikamwambia mechi ya Kesho kama unataka kucheza utacheza, lakini najua haupo fiti, mimi ni kocha najua wachezaji wangu, lakini sikushauri acheze kwa sababu nilijua kitakachotokea, na kweli baada ya mechi tulipoteza kwa 1-5.” Alisema Cadena.

Ifahamike kwamba Mkataba wa Dani Cadena Simba ulimalizika Juni 30, na hadi sasa hakuna mazungumzo yaliyofanyika kwa kocha huyo.

SOMA NA HII  MCHEZAJI MAMELODI APATWA NA KICHAA...ANAISHI CHINI YA DARAJA...INASIKITISHA SANA