Home Habari za Yanga Leo MANARA AMFUKUZISHA KAZI ALI KAMWE YANGA

MANARA AMFUKUZISHA KAZI ALI KAMWE YANGA

Habari za Yanga- Ali Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe ametangaza kuachia nafasi hiyo huku akisema muda wake umemalizika.

Kamwe aliyehudumu katika nafasi hiyo kwa miaka miwili amethibitisha kuondoka Yanga kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram leo Jumapili Julai 28, 2024.

“A Good dancer must know when to Leave a Stage.

“𝑀𝑡𝑢𝑚𝑏𝑢𝑖𝑧𝑎𝑗𝑖 𝑚𝑧𝑢𝑟𝑖 𝑎𝑛𝑎𝑡𝑎𝑘𝑖𝑤𝑎 𝑘𝑢𝑗𝑢𝑎 𝑛𝑖 𝑤𝑎𝑘𝑎𝑡𝑖 𝑔𝑎𝑛𝑖 𝑤𝑎 𝑘𝑢𝑜𝑛𝑑𝑜𝑘a 𝐽𝑢𝑘𝑤𝑎𝑎𝑛𝑖..”

“Maneno ya hekima kutoka katika kinywa cha Patrick Loch Otieno Lumumba;

“Na ni Hekima hii, inanituma mbele yenu Wananchi, Mashabiki na Wanachama wa Klabu yetu pendwa, kuwaambia kuwa, Ni wakati sasa wa kijana wenu kuondoka Jukwaani.

“Nimesimama Miaka miwili juu ya hili Jukwaa, Tumeimba, Tumecheza, Tumefurahi na Alhamdulillah Tumeshinda pamoja kila pambano Lililokuja mbele yetu.

“Muda wangu umemalizika na Asanteni sana.

“Tutaonana tena Wakati mwingine nikiwa na kitu kizuri cha kuwaonyesha Juu ya Jukwaa.” Aliandika Ali Kamwe.

Haji Manara wakati akifanya mahojiano na waandishi wa habari katika siku yake ya kutangaza kumaliza adhabu yake ya TFF, alipoulizwa ni kwa jinsi gani atakwenda kufanya kazi klabuni hapo ikizingatiwa kuwa majukumu anayokusudia kwenda kufanya kwa sasa yanafanywa na Ali Kamwe (Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC).

Manara alijibu kuwa yeye ndiye msemaji wa Yanga SC na kwamba kabla hajafungiwa amefanya kazi kwa takribani mwaka mmoja (1) na Hassan Bumbuli (Aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga SC) bila kuingiliana kwenye majukumu kwa kuwa kila mtu alifanya majukumu yake, hivyo ni matumaini yake kuwa hata kwa waliopo sasa itakuwa hivyo.

Manara amekanusha madai ya kuwa Ali Kamwe ni ‘Boss’ wake badala yake ameendelea kutoa msisitizo kwa wanahabari na Watanzania kwa ujumla kufahamu kuwa wawili (2) hao kila mmoja anatimiza majukumu yake.

“Mimi nafanya kazi na mtu yeyote yule, Ofisa Habari sio Boss wa Idara, narudi Yanga SC kama Msemaji wa klabu na interest yetu ni mpira na sio kwenda kuchukua kazi za watu.

SOMA NA HII  SIMBA NA YANGA KUOGA MAMILIONI YA CAF

“Niko tayari kuitumikia klabu yangu ya Yanga, niliiacha nikiwa msemaji baada ya kufungiwa na bila shaka Yanga wataniambia unakwenda kuwa nani, tusubiri viongozi, kamati ya utendaji irejee, hilo ni jukumu lao sio langu,” alisema Manara.