Home Habari za Yanga Leo MIGUEL GAMONDI…KAWEKA WAZI KIKOSI CHAKE.

MIGUEL GAMONDI…KAWEKA WAZI KIKOSI CHAKE.

Habari za Yanga- Gamondi

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amesema licha ya usajili wa mastaa waliosajiliwa katika timu hiyo, hana hofu ya kupanga kikosi.

Gamondi amesema kikosi kitakuwa kinapangwa kulingana na aina ya wapinzani wanaokutana nao.

Amesema mbali na wapinzani, pia itategemea na viwango vya wachezaji ili kutumika kwenye michezo husika.

“Ugumu wa kupanga timu? Hapana. Hakuna ugumu, timu inapangika sioni wasiwasi kabisa, inategemea na mpinzani utakayekutana naye,” amesema Gamondi.

“Mimi sio mtu ninayepanga timu kwa kuangalia majina ya wachezaji, inategemea kiwango cha mchezaji. Kuna wakati utahitaji kucheza na viungo wawili wakabaji, wakati mwingine washambuliaji wawili, wakati mwingine viungo washambuliaji wawili au watatu.

“Kuna wakati unaweza kumpa nafasi Azizi (Stephanie) acheze, ukampumzisha mwingine au wakati mwingine ukawatumia wote, ligi ni ndefu na mechi ni nyingi.”

Yanga ilimaliza Ligi Kuu Bara msimu uliopita ikiwa bingwa wa mashindano hayo na Kombe la Shirikisho (FA).

Klabu ya Yanga mpaka sasa wamefanikiwa kukamilisha sajili za wachezaji  wenye majina makubwa kama Clatous Chama akitokea Simba, ila amesajiliwa kama mchezaji huru.

Chadrack Boka beki wa kushoto ambaye ni mrithi wa Joyce Lomalisa, na Abubakar kHOMEINY Mlinda mlango mrithi wa Metacha Mnata aliyesajiliwa na Singida Blak Stars. Na Mwana Mfalme Prince Dube ambaye alivunja mkaaba wake na klabu ya wauza Ice Cream Azam FC.

Wchezaji wengine wanaopewa nafasi ya kuja kujiunga na Yanga kwa msimu ujao ni Jean Baleke ambaye aliwahi kupita Simba, kabla ya kujiunga na Al Ittihad ya Libya ambako alikuwa mfungaji bora.

Baleke anachukua nafasi ya mshambuliaji Jonathan Sowah ambye alikuwa anahusishwa zaidi na Yanga, lakini Uongozi ukaona ukimsajili Jean Baleke basi tatizo  lao la washambuliaji litapa suluhisho.

Moja kati ya mastaa waliopo Simba kwa sasa ni Aziz Ki ambaye hivi karibuni alizua sintofahamu baada ya kusemekana bado hajaongeza mkataba na timu yake ya sasa. Ila Jana Julai 10 amethibitisha kwamba aaendelea kukipiga katika klabu hiyo.

SOMA NA HII  ANDABWILE NI MALI YA YANGA...YANGA YAIJIBU SIMBA