Home Habari za Simba Leo SUALA LA MANULA NGOMA NGUMU SIMBA

SUALA LA MANULA NGOMA NGUMU SIMBA

Habari za Michezo

BADO kesho ya golikipa Aishi Manula haieleweki ndani ya Simba Kwa kuwa mpaka Sasa hajaungana na wenzake Pre- Season inayoendelea Misri.

Taarifa zinadai kuwa, ni kama viongozi hawaoni Sababu ya kuendelea naye tena lakini hofu Yao ni Kwamba asije akaenda timu zingine ikiwemo Azam FC ambao wapo mstari wa mbele kutaka kumrejesha.

Hadi Sasa Manula ameshapona majeraha yake na yupo tayari kuitumikia klabu yake ingawa bado Kuna giza.

Mchezaji huyo bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Simba na Simba wanajifikiria mustakabali wa Kipa huyo, kama aendelee kuwepo au wamuache akapate changamoto nyingine.

Klabu ya Azam FC inaelezwa kwamba imeiandikia barua Uongozi wa Simba kuhitaji huduma ya mlinda mlango wao Aishi Manula.

Lakini hadi sasa Uongozi wa klabu hiyo bado hawajaijibu barua hiyo, kwa taarifa zilizopo kutoka ndani ya klabu ya Simba ni kwamba Aishi Manula yupo kwenye mahesabu ya kumtoa kwa mkopo kipa huyo, au kumuuza moja kwa moja.

Alipohojiwa na Azam Media Ahmed Ally alisema kwamba msimu ujao watakuwa na makipa wao akiwataja kwa majina, Lakred, Ally Salim na Hussein Abel lakini jina la Aishi Manula hakulitaja.

“Bila shaka unamzungumzia Aishi Manula, ni taarifa hata mimi binafsi nimeziona mitandaoni ila sijapewa taarifa kutoka kwa Viongozi wangu, bado ana mkataba wa mwaka mmoja siwezi kusema kama ntutaomtoa kwa mkopo au tutamuuza, lakini nithibitishe kwamba Ayub Lakred tunae, Ally Salim tunae na Hussein Abel yupo.” Alisema Ahmed Ally

Soka La Bongo tuliripoti juu ya taarifa za kuhitajika kwa Aishi Manula na klabu ya Azam FC, lakini hadi sasa Uongozi wa timu hiyo umekuwa ukificha sana taarifa za mlinda mlango huyo.

Azam FC wanataka kuimarisha timu yao kuelekea kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao, hivyo wanahtaji wachezaji wakubwa na wazoefu na wanaamini uzoefu na ukomavu wa kipa huyo namba moja wa Taifa Stars utaenda kuwasaidia sana kwenye timu kufikia malengo yao.

SOMA NA HII  USHINDANI WA MASTAA HAPO SIMBA SIO POA, MATOLA AMUIBIA SIRI MIQUISSONE