Home Habari za Simba Leo WAKALA WA MPANZU AFUNGUKA KILICHOKWAMISHA…USAJILI WA MTEJA WAKE SIMBA

WAKALA WA MPANZU AFUNGUKA KILICHOKWAMISHA…USAJILI WA MTEJA WAKE SIMBA

Habari za Simba SC- ELLIE MPANZU
Mchezaji wa AS Vita Elie Mpanzu Anayehusishwa kujiunga na klabu ya Simba SC msimu ujao wa 2024/25

BAADA YA Dili la Kuinasa saini ya Winga wa AS Vita Ellie Mpanzu kugonga mwamba  katika mita ya Msimbazi, Wakalawa mchezaji huyo Raia wa DR Congo Papida amefunguka kilichokwamisa usajili huo.

Akizungumzia usajili wa mchezaji anayemsimamia Ellie Mpanzu wakalahuyo alisema kwamba,  usajili wa Simba haueleweki unafanywa na nani,  huku akienda mbali zaidi kuilinganisha timu hiyo na watani zao Yanga,  akiusifu usajili wao.

“Tofauti ya Simba na Yanga ni kuwa Yanga wanapotaka Mchezaji unawasiliana na Mtu mmoja tu ila Simba watu ni wengi sana kwa dili moja, mara Salim, mara Mulamu mara Magori na pia walikuja kwa kuchelewa sana kuhusu kumtaka Mchezaji wangu Ellie Mpanzu, hata hivyo hawezi kwenda Simba anaenda Ulaya, lakini nilishawaambia Simba ipo siku watanitafuta, nitawapa Wachezaji wakishanilipa pesa yangu dola 5,000 kuna dili tulifanya na wanajua” Alisema Papida wakala wa Ellie Mpanzu.

Lakini  pia alieleza namna nzuri ya kufanya usajili wa wachezaji wazuri ambayo,  hata Simba aliwahi kuwashauri wafanye.

“Simba hawana sera nzuri ya kutafuta Wachezaji, wanapaswa kuelewa Congo ama Afrika ina Wachezaji wengi wazuri sana, ila unapaswa kuwachukua wakiwa na umri mdogo niliwapa ushauri wachukue Wachezaji wa miaka 15-17 wapikwe kwenye mifumo yao watakuja kuwa wazuri sana baadae, hawataki wanataka wachezaji ambao wameshakomaa hiyo sio sera nzuri, kwa Tanzania Simba ni timu yangu, mimi sishabikii Yanga”

Simba na AS Vita walishindwa kufikia makubaliano ya kuuziana mchezaji huyo, huku ikidaiwa kwamba AS Vita waliweka kigingi kumruhusu mchezaji wao wakati huo Simba wakiihitaji zaidi saini ya Mpanzu.

SOMA NA HII  KISA MATOKEO YA SARE JANA...AHMED ALLY AIITA YANGA 'WACHAWI UNITED'...ADAI WAMEFUKIA HIRIZI...