Home Habari za Yanga Leo YANGA KUCHEZA NA GOR MAHIA YA KENYA…WIKI YA WANANCHI HIYOOO

YANGA KUCHEZA NA GOR MAHIA YA KENYA…WIKI YA WANANCHI HIYOOO

HABARI ZA YANGA-GAMONDI

Klabu ya Gor Mahia Imetuma mualiko kwa klabu ya Yanga kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa mwishoni mwa mwezi huu.

Mechi hiyo ni mahususi kwa ajili ya ufunguzi wa uwanja mpya wa Siaya County uliopo nchini Kenya.

Yanga imekubali mualiko huo wa Gor Mahia na imeshaipa taarifa Gor Mahia kuwa watacheza mchezo huo.

Lakini pia kambi ya Yanga ipo pale pale Avic Town na inaelezwa kwamba watasafiri kwenda kushiriki mashindano waliyoalikwa Afrika Kusini.

Huko watacheza dhidi ya Kaizer Chief na klabu ya Bundasliga FC Augsburg ikiwa ni mechi za kirafiki.

Katika usajili wa dirisha kubwa msimu huu Klabu ya Yanga hadi saa imetambulisha wachezaji wapya 6, ambapo Clatous Chama, Prince Dube, Chadrack Boka, Abubakar Khomeiny Mlinda mlango, Kiungo Duke Abuya na Azizi Andabwile.

Lakini huenda kukawa na usajili mwingine wa mchezaji aliyewahi kukipiga mitaa ya Msimbazi kwa misimu miwili.

Jean Othos Baleke ameonekana kwa nyakati tofauti akiwa kambi ya Yanga akifanya mazoezi na wenzake, na ndiyo usajili unaopewa nafasi kubwa ya kurithi viatu vya Fiston Mayele.

Baada ya Mayele kuondoka Yanga, Wananchi wamefanya usajili wa washambuliaji 6 hadi sasa, kuna Hafiz Konkoni, Joeseph Guede, Kennedy Musonda, Clement Mzize, Prince Dube na Jean Othos Baleke.

Kwa upande wa mashabiki wa Yanga wenyewe wanaisubiri siku ya Kilele cha Wiki ya Mwananchi Agosti 4, tayari  kabisa kulishuhudia jeshi  lao   la  msimu ujao  2024/25.

SOMA NA HII  KUHUSU BOBOSI KUJA LINI YANGA SC...UKWELI HUU HAPA...ALLY KAMWE 'AROPOKA.'..