Home Habari za Simba Leo SIMBA YAWEKA REKODI NYINGINE AFRIKA…KWA MKAPA FULL HOUSE

SIMBA YAWEKA REKODI NYINGINE AFRIKA…KWA MKAPA FULL HOUSE

HABARI ZA SIMBA

KUELEKEA Agosti 3 Katika Tamasha kubwa la Michezo Afrika la Simba Day uongozi wa Simba umebainisha kuwa mashabiki wamefanya jambo kubwa ambalo linastahili pongezi kwa kununua tiketi zote za tamasha hilo linalosubiriwa kwa shauku kubwa kwenye ulimwengu wa michezo.

Mtendaji Mkuu wa Simba Imani Kajula amewashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa kufanikisha jambo hilo kwa kununua tiketi zote licha ya kuwa na madaraja tofautitofauti.

Akizungumzia kufikia tamati kwa uuzaji wa tiketi Kajula amesema kuwa Simba wameonyesha ukubwa kwa kuvunja rekodi ya mwaka tofauti.

โ€œSimba tumeonyesha ukubwa wetu na tumeweza kuvunja rekodi yetu ya mwaka jana ambapo tuliuza tiketi zote siku mbili kabla ya Simba Day, mwaka huu tumeuza tiketi zote โ€“ SOLD OUT siku tatu kabla ya Simba Day.

โ€œHongereni sana mashabiki wetu na tukutane uwanja wa mkapa kwenye Simba Day ya Ubaya Ubwela. Timu yeyote kubwa inapimwa na ukubwa wa sapoti ya mashabiki wake, na hii inadhihirisha kwanini mashabiki wa Simba mlichaguliwa kuwa mashabiki bora barani Afrika.โ€

Agosti 3 2024 itakuwa ni utambulisho wa wachezaji wapya na wale waliokuwa na timu kwa msimu wa 2023/24 miongoni mwao ni pamoja na Mzamiru Yassin,Mohamed Hussein, Ayoub Lakred.

SOMA NA HII  MO DEWJI AMKATAA LOMALISA...AANZA NA LAKRED