SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa Orodha mpya ya Vilabu Bora Afrika kuelekea msimu mpya 2024/25.
Miongoni mwa Vilabu bora kwa sasa Afrika, Simba inashika nafasi ya 7 kwa ubora huku ikiwa ndiyo timu pekee iliyoingia 10 bora kwa timu za Afrika Mashariki.
Licha ya ubora mkubwa walionao Yanga kwa sasa, lakini wameshindwa kupenya kwenye viwango vikubwa vya CAF kwa timu 10 za juu.