Home Habari za Yanga Leo AZIZ KI ATOA NENO KABLA YA KILELE CHA WANANCHI

AZIZ KI ATOA NENO KABLA YA KILELE CHA WANANCHI

HABARI ZA YANGA- AZIZ KI

BAADA ya kutwaa tuzo nne za msimu uliopita, kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki amesema anajisikia kubarikiwa huku akimtaja kocha wa timu hiyo, Miguel Gamondi kuwa amehusika kwa asilimia kubwa.

Aziz Ki amepata tuzo ya mfungaji bora, kiungo bora, mchezaji bora na ni mmoja wa wachezaji wanaounda kikosi bora cha msimu 2023/24.

Mchezaji huyo bora wa msimu amesema Gamondi na maono yake ndiyo yamewafanya kuwa kwenye kiwango cha ushindi na ametumia nafasi hiyo kumshukuru kwa juhudi zake.

“Kwa kocha wetu kipenzi Gamondi, kwa kushirikiana na benchi la ufundi lote asante sana kwa kuhakikisha mnatuweka sawa kucheza, na kwa wafanyakazi wote wa Yanga, asanteni kwa juhudi zenu zisizo na kikomo,” amesema.

“Najisikia kubarikiwa sana nashukuru kwa safari ya ajabu na utambuzi niliopokea jana, kwanza kabisa, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa baraka zake za kila mara, familia yangu kutokana na maombi yao na usaidizi usioyumba unamaanisha kila kitu kwangu.

“Shukrani za dhati kwa Serikali chini ya utawala wa Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya michezo nchini Tanzania. Pia nalishukuru Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kuandaa tuzo hizi na maono yako wazi ya ukuaji wa soka Tanzania.”

Pia ameushukuru uongozi wa Yanga, chini ya rais Hersi Said ambaye anapambana kuhakikisha timu inafanya vizuri na kukua kila wakati.

Aziz Ki amewashukuru wachezaji wenzake akiweka wazi kuwa sapoti yao ni muhimu na anawapenda na kupongeza kwa kuifanya timu hiyo kuwa ya ndoto kwa wachezaji wengi, huku akiwawashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa sapoti wanayoitoa kwao.

SOMA NA HII  BAADA YA 'KUPASUKA' KWA AZAM FC...GAMONDI AVUNJA UKIMYA YANGA...ATAJA ALIYEWAMALIZA...