Home Habari za michezo BAADA YA KUANZA KUTUPIA YANGA….CHAMA KATUPA DONGO HILI KWA SIMBA….

BAADA YA KUANZA KUTUPIA YANGA….CHAMA KATUPA DONGO HILI KWA SIMBA….

Chama Yanga

BAADA ya kufunga bao lake la kwanza la Ligi ya Mabingwa Afrika, Kiungo wa Yanga, Clatous Chama amesema ataendeleza rekodi ya kufunga mabao na kutengeneza nafasi katika michuano hiyo kwa msimu wa 2024/25.

Chama anahitaji kuendelea alipoishia msimu uliopita kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika , Chama akiwa Simba amefunga bao moja na ‘assist’ moja.

Kiungo huyo msimu huu anaitumikia Yanga nakatika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vital’O ya Burundi alifunga bao moja na ‘assist’ moja, timu yake ikishinda mabao 4-0.

Kiungo huyo  amesema kuwa, anafurahi kufunga bao lake la kwanza akiwa ndani ya kikosi cha Yanga na kuendeleza rekodi ua ufungaji wa mabao katika michuano hiyo.

Amesema ushindi walioupata dhidi ya Vital’O ni mkubwa sana na anaimani kwa ubora wa timu yao ataendelea kufanya vizuri na kuendeleza rekodi yake kwenye michuano ya kimataifa.

“Malengo yangu ni kuendeleza rekodi yangu ya kufunga katika kila mechi kwenye hii michuano na Yanga kufikia kile wanachokitarajia ikiwemo kucheza fainali ya Afrika.

Kwa ubora uliopo ndani ya Yanga ninamatarajio makubwa ya kufikia huko kwa sababu kila mchezaji anataka kucheza fainali hiyo,” amesema Chama.

SOMA NA HII  BAADA YA KIMYA KIREFU....AJIBU KASHINDWA KUJIZUIA...KAIBUKA NA HILI JIPYA KWA TIMU YAKE...