Home Habari za Yanga Leo CLEMENT MZIZE AWAJIBU WANAOMPONDA…NAUMIA KUKOSA NAFASI

CLEMENT MZIZE AWAJIBU WANAOMPONDA…NAUMIA KUKOSA NAFASI

HABARI ZA YANGA-MZIZE

BAADA ya Maneno kuwa mengi sana Mtandaoni kuhusu Mshambuliaji wa Yanga Clement Mzize kutotumia nafasi anazopata. Mchezaji huyo amefunguka kwa kuwanyamazisha mashabiki.

Mzize amekuwepo Yanga kwa misimu mitatu sasa huku akiwa tumaini la Wanayanga baada ya Mayele kutimikia Misri kwenye Klabu ya Pyramids FC.

Msimu uliomalizika Yanga wamefanikiwa kutoa mfungaji bora wa Ligi KUU ya NBC, ambaye ni Aziz Ki lakini kwa upande wa Mzize ameendelea kutupiwa lawama kila siku.

Mchezaji huyo amefunguka hali hiyo inavyomtesa na alivyoipokea huku akitoa ahadi ya kufanya poa sana kwa msimu ujao wa 2024/25.

“Maneno ni mengi kunihusu hasa nikikosa nafasi ya kufunga mimi pia naumia lakini napata nguvu kutoka kwa Gamondi ambaye siku zote amekuwa akiniambia mimi ni bora na natakiwa kuonyesha bila kujali ukiachana na maneno yake amekuwa akiendelea kunipa nafasi,” alisema Mzize na kuongeza,

“Nafikiri kuendelea kuaminiwa na kupewa nafasi ndio siri.”

SOMA NA HII  MASTAA YANGA SC WATUA KISHUA NIGERIA....RIVER UNITED WAPAGAWA...