Home Habari za Yanga Leo MIGUEL GAMONDI KUHUSU COMBO YA DUBE, MZIZE

MIGUEL GAMONDI KUHUSU COMBO YA DUBE, MZIZE

habari za Yanga- Mzize

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema ni mapema, lakini amefurahishwa na pacha iliyotengenezwa na Prince Dube wakishirikiana na Clement Mzize akiwataja kuwa wanamuofa vitu vingi uwanjani.

Wawili hao kwenye mechi tatu za kirafiki zilizochezwa na Yanga, kule Sauzi walianza pamoja kwenye mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs timu hiyo ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Mbali na mchezo huo Yanga ilicheza na TS Galax wakishinda bao 1-0, Dube alianzia benchi huku Mzize akianza kikosi cha kwanza na mechi ya tatu ilikuwa ni dhidi ya FC Augsburg ambao pia Dube aliingia akitokea benchi.

Kwenye mechi hizo tatu washambuliaji hao kila mmoja amefunga bao moja kwenye mchezo walioanza pamoja dhidi ya Kaizer Chiefs timu hiyo ikitwaa taji baada ya ushindi wa mabao 4-0.

Akizungumza na Mwanaspoti, Gamondi alisema ana kikosi kizuri na kila mchezaji anaonyesha ubora lakini amefurahishwa namna Dube na Mzize wameweza kuelewana kwa uharaka.

“Dube na Mzize wamecheza pamoja mechi zote tatu japo kuna mbili mmoja kaanzia benchi lakini mara baada ya kuwa wote uwanjani wamekuwa wakicheza vizuri kwa kuelewana,” alisema na kuongeza;

“Wawili hao bila ya kuelekezwa wamekuwa wakibadilishana upande kiwandani kwa kuingia ndani ya 18 wakitokea pembeni na wana uwezo sawa kwenye mashambulizi na kukaba wananipa vitu viwili tofauti kiwanjani.”

Gamondi alisema anaelewa juhudi za Mzize kiwanjani hasikilizi maneno ya mashabiki ataendelea kumtumia kwasababu kile anachomuelekeza anafanya huku akiweka wazi kuwa suala la kufunga hakuna mchezaji anafundishwa inatokea tu.

“Mbinu zote ninazomuelekeza anazifanya na amekuwa mchezaji ambaye anafanya mambo mengi uwananjani huwa sisikilizi nini kinasemwa naangalia nini kinafanyika na ndio maana nimekuwa nikimtumia, mechi zote tatu ameanza sababu ni anafanya kazi yake,” alisema na kuongeza:

“Mzize ni mchezaji ambaye ni nadra sana kuwa naye kikosini kwani anauwezo wa kutumia miguu yote miwili hivyo ni rahisi kwake kukaa kwenye maeneo bila kujali mguu gani atatumia wakati huo.”

SOMA NA HII  KIUNGO MNIGERIA AWAGOMEA SIMBA...MABOSI WACHANGANYIKIWA