Home Habari za michezo FISTON MAYELE AKOSA UFUNGAJI BORA

FISTON MAYELE AKOSA UFUNGAJI BORA

HABARI ZA YANGA- mAYELE

Mshambuliaji wa Klabu ya Pyramids ya nchini Misri Fiston Kalala Mayele ameshindwa kuwa mfungaji wa Ligi Kuu ya Misri mara baada ya kufanikiwa kufunga magoli 17.

Mbio za ufungaji bora katika Ligi Kuu ya Misri zilikuwa kati ya Mayele na Wesam Abou Ali wa Al Ahly aliyefunga goli 18 huku Mayele akiwa amefunga goli 17.

Tayari klabu ya Pyramids wamemaliza mechi za Ligi Kuu ya Misri (34) ambapo mabingwa Al Ahly wao wana mechi moja mkononi na tayari Wesam Abou Ali amekuwa mfungaji bora.

Kumbuka kipindi ambacho Fiston Mayele anacheza Ligi Kuu ya Tanzania katika klabu ya Yanga amewahi kuwa mfungaji bora msimu wa 2022/2023.

SOMA NA HII  KAULI ZA KIBABE, MASHABIKI WA SIMBA WAJIMALIZA