Home Habari za michezo PAMOJA NA KUWAKANDA VITAL’O GOLI 6-0…MUDATHIR AFUNGUKA ‘BIFU LAKE’ NA GAMONDI…

PAMOJA NA KUWAKANDA VITAL’O GOLI 6-0…MUDATHIR AFUNGUKA ‘BIFU LAKE’ NA GAMONDI…

Yanga SC LEO

KIUNGO wa Yanga, Mudathir Yahya ameweka wazi ubishi kati yake na kocha wa timu hiyo Miguel Gamondi katika mchezo wa marudiano wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vital’o ya Burundi.

Amesema alipokuwa benchi walibishana na kocha wake huyo kuhusu mechi hiyo watafunga idadi ya mabao 8 ambapi Gamondi alidai haiwezi kufika huko.

Mudathir amesema kabla ya mechi hiyo aliamini watafunga zaidi ya mabao 8 kulingana na maandalizi lakini Gamondi aliweza kubishana na nyota huyo.

“Nikiwa benchi kabla sijaingia kulikuwa na ubishi na kocha kuwa tunashinda mabao 8, kocha akanifuata na kuniambia haya sasa zamu yangu kuingia kwenda kutafuta bao mbili ili kutimiza idadi hiyo.

Nashukuru Mungu nilifanikiwa kufunga bao moja na kutimiza idadi ya mabao 6-0, tofauti na kile nilichotarajia na kocha Gamondi amefanikiwa kunishinda katika ligi yetu ya idadi ya mabao katika mchezo huu,” amesema kiungo huyo.

Ameongeza kuwa msimu huu wana kikosi imara zaidi ya uliopita na wananchi watatajie kuona viungo na washambuliaji wanaingia vita vya kuwania ufungaji bora.

“Safari hii viungo na washambuliaji tunashinda wenyewe kwa wenye maana kila mtu atafunga sana kwenye ligi na hata michuano ya kimataifa, asipofunga Dube (Prince) na Mzize (Clement), atafunga Aziz Ki (Stephen), Chama (Clatous) au nitafunga mimi,” amesema kiungo huyo aliyeweka wazi kuitaka fainali ya Afrika.

SOMA NA HII  YANGA YAJIAPIZA KUNOGESHA UZINDUZI WA CAF.