Home Habari za michezo RASMI….MOSES PHIRI ‘AJIONDOA’ SIMBA SC…ISHU NZIMA IKO HIVI…

RASMI….MOSES PHIRI ‘AJIONDOA’ SIMBA SC…ISHU NZIMA IKO HIVI…

Moses Phiri ajiondoa Simba SC

WAKATI wachezaji wa Simba SC wakiwa wanajiandaa kwa ajili ya kuelekea Zanzibar kushiriki Mapinduzi Cup imebainika kuwa straika wa timu hiyo, Mzambia Moses Phiri amejiondoa kikosini kwa kurejea kwao.

Phiri amerudi Zambia kwa ajili ya mapumziko huku pia akiwa anauguza jeraha lake la kifundo cha mguu alilolipata katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar.

Taarifa tayari zilithibitisha kuwa Phiri atakosekana ndani ya Simba SC kwa kipindi cha wiki nne jambo ambalo ni wazi kuwa ataikosa michuano ya Mapinduzi inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho Jumapili.

Phiri alithibitisha juu ya kurejea kwao kwa mapumziko huku akiwa anauguza majerha yake ambayo anamini kuwa muda si mrefu atarejea uwanjani.

“Ni kweli natarajiwa kwenda nyumbani Zambia kwa ajili ya mapumziko na kuuguza mguu wangu ambao nimeumia katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar tukiwa ugenini, naamini mapumziko ambayo nitayapata pia yatanisaidia kupona haraka na kurejea tena uwanjani.

“Kwa mashabiki wangu na wale mashabiki wa Simba SC wazidi kuniombe ili nipone haraka na nirejee kuwatumikia na kuwapa raha zaidi, hivyo kwa sasa ni kuwatakia tu usindi katika kila michezo ambayo watacheza mimi nikiwa sipo na naamini watafanya vyema,” alisema Mzambia huyo.

SOMA NA HII  KUELEKEA MICHAUNO YA CAF...PABLO ASHANGAZA UMAA..HAJUI LOLOTE...AMTAJA CHAMA TENA...