Home Habari za michezo π†πŽπ‹πˆ 𝐋𝐀 π”π†π„ππˆππˆ πŒπ€π’π‡πˆππƒπ€ππŽ π˜π€ 𝐂𝐀𝐅 πŠπ”π…π”π“π–π€.

π†πŽπ‹πˆ 𝐋𝐀 π”π†π„ππˆππˆ πŒπ€π’π‡πˆππƒπ€ππŽ π˜π€ 𝐂𝐀𝐅 πŠπ”π…π”π“π–π€.

habari za simba na yanga

Kuelekea Msimu ujao Wa mashindano ya CAF champions league Pamoja na CAF Confederation League Kamati ya Mashindano ya CAF Iko kwenye majadiliano juu ya Kufuta Sheria ya Goli la Ugenini 2024/25.

Kwa kipindi cha miaka mingi wadau wa soka la Afrika wamekuwa wakilalamikia juu ya kanunia hiyo ya goliΒ  la ugenini kwenye mashindano hayo.

Goli la ugenini limezinyima mafanikio timu nyingi ikiwemo Simba na Yanga kwa nyakati tofaouti,Β  itakumbukwa kwa mara ya kwanza Yanga anahukumiwa juu ya goli la ugenini alicheza fainali ya Kombe la Shirikisho na akapoteza Kombe hilo.

Hata kwa Simba pia amehukumiwa na goli la ugenini, alipokuwa Afrika Kusini mchezo wa kufuzu nusu fainali,Β  na hata mashindanoΒ  Β ya AFL dhidi ya Al ahly, Ligi ya Mabingwa Afrika pia dhidi ya Wydad Casablanca.

Kikao hicho kitakuja na mrejesho kuhusu makubaliano, lakini asilimiaΒ  kubwa imeonekana kutoridhishwa na kanuni hiyo ambayo hata Ulaya walishaifuta.

SOMA NA HII  SPIDER MAN ATAMBULISHWA SIMBA...LAKRED THANK YOU