HABARI ZA YANGA-GAMONDI
Habari za Yanga Leo

GAMONDI AWAONYA MASTAA WAKE…WASIJISAHAU

Abubakar September 11, 2024 11:14 am

Licha ya kikosi chake kuonyesha ubora mkubwa katika mechi za mwanzo msimu huu, Kocha Mkuu wa Yanga SC Miguel Gamondi amesema haimaanishi kama wako salama na itakuwa rahisi kwao kupata mafanikio kama ilivyokuwa msimu uliopita.

Gamondi amesema msimu huu anatarajia kupata upinzani mkali zaidi kutoka kwa wapinzani wao katika michuano yote wanayoshiriki kwani kila timu inajiandaa kwa lengo la kushindana na Yanga Sc.

“Kila timu sasa inataka kuifunga Yanga SC, inabidi tupambane, tusijidangaye kuwa tupo kwenye mstari salama, ninawaambia haya hata wachezaji wangu, wanatakiwa kila siku waongeze juhudi na mazoezi zaidi ili tuwe bora kila kukicha kwani wenzetu nao wanaongeza ubora ili watufikie au watupite.”

MUDATHIR ATEMA NYONGO WANAOPONDA WACHEZAJI WAZAWA NANI KAMA MOHAMMED HUSSEIN…MIAKA 15 KWENYE UBORA ULE ULE