HABARI ZA YANGA-Injinia Hersi
Habari za Yanga Leo

YANGA YAZITAKA TATU ZA KENGOLD FC

Abubakar September 25, 2024 10:50 am

MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ken Gold unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya na kikubwa ni pointi tatu muhimu wanahitaji.

Mchezo huo ni wa pili kwa Yanga ambao ni mabingwa watetezi ikumbukwe kwamba mchezo wa kwanza ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar, ulichezwa Uwanja wa Kaitaba, baada ya dakika 90 ubao ulisoma Kagera Sugar 0- 2.

Yanga mabao yakifungwa na Clement Mzize na Maxi Nzengeli ambaye ni mfungaji wa bao la kwanza ndani ya Yanga msimu wa 2024/25.

Gamondi amesema: “Tunatambua mchezo hautakuwa mwepesi kuwakabili wapinzani wetu Ken Gold tunawaheshimu na tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu kikubwa ni kuona kwamba tunapata pointi tatu muhimu kwenye mchezo wetu.

“Siku zote timu yoyote ikicheza na Yanga wanakuwa makini na kutafuta matokeo kama sisi, tutacheza kwa tahadhari na tuna wachezaji wazuri wenye uzoefu wa kucheza kwenye mazingira yoyote.”

Ken Gold baada ya kucheza mechi nne ambazo ni dakika 360 haijaambulia ushindi katika mechi zake za msako wa ushindi ndani ya uwanja ikiwa imepanda ligi msimu wa 2024/25.

WALA SIMBA HAIWAOGOPI AZAM HATA KIDOGO KUHUSU SIMBA , YANGA KUFUZU KIMATAIFA…FAIDA MPYA KWA TANZANIA HIZI HAPA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

One response to “YANGA YAZITAKA TATU ZA KENGOLD FC”

  1. […] wa Yanga umewaingiza kwenye mtego wapinzani wao KMC kuelekea kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa […]