Home Habari za Yanga Leo GAMONDI AMALIZA UTATA… SIMCHUKII BALEKE

GAMONDI AMALIZA UTATA… SIMCHUKII BALEKE

Habari za Yanga leo

Kocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amemaliza utata kwa kutoa sababu zinazomfanya mshambuliaji mpya, Jean Baleke aliyeibua maswali kwa mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo kwa kutoonekana uwanjani.

Gamondi alisema hatua zinafanyika kwa sasa za kumboresha ambazo zimeanza muda mrefu, kwani kwanza walikuwa wanampambania apungue kidogo uzito jambo linaloendelea vizuri kwa sasa, kwa kuwa alikuwa mzito kiasi cha kushindwa kuendana na kasi ya benchi la ufundi ndio maana wenzake wanaendelea kukipiga.

“Baleke yuko na programu maalum ili kumuongezea wepesi wa kufanya uamuzi akiwa karibu ya lango na kufunga zaidi ya alivyozoeleka, Pia mjue kabisa Baleke ni mahiri zaidi kwa kufunga mabao ya kichwa kuliko miguu, ndio maana tunaendelea kumpa mazoezi awe vizuri kotekote,” alisisitiza Gamondi na kuongeza;

“Mshambuliaji mzuri ni yule ambaye anaweza kufunga kwa mipira ya aina zote juu na chini, kwani kazi yake kubwa ni kuipa timu matokeo ndio maana tunamnoa zaidi, lakini sio kama nina tatizo naye, wachezaji wote kwangu ni wachapakazi, kikubwa natafuta matokeo zaidi kuliko jina la mtu.” Alisema Miguel Gamondi.

SOMA NA HII  BAKARI MWAMNYETO NA SIMBA...MAMBO YAMEKUWA MAMBO