Home Habari za michezo HALMASHAURI KUJENGA VIWANJA VYAO…SIMBA NA YANGA VICHEKO TU

HALMASHAURI KUJENGA VIWANJA VYAO…SIMBA NA YANGA VICHEKO TU

HABARI ZA MICHEZO

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo inafikiria kuzielekeza Mamlaka bajeti zao kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ujenzi wa viwanja vya michezo kwa maeneo yao.

Hayo yamesemwa leo Septemba 3,2024 na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Jacqueline Kainja.

Mbunge huyo amehoji Serikali ina mpango gani wa kujenga viwanja vya michezo nchini katika ngazi ya wilaya.

Akijibu swali hilo, Mwinjuma amesema jukumu la ujenzi wa miundombinu ya michezo ni la Serikali kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya michezo zikiwemo taasisi, mashirika, watu binafsi na mamlaka za Serikali za Mitaa.

Amesema katika kuhakikisha kuwa kila wilaya inakuwa na viwanja vya michezo, karibuni Serikali itazielekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa kutenga mafungu katika bajeti zao ili kutekeleza miradi ya ujenzi wa viwanja vya michezo kwa maeneo yao.

“Tayari kuna halmashauri zimeanza utekelezaji huu ambazo ni:- Halmashauri za Wilaya za Kinondoni (Uwanja wa KMC Stadium), Bukoba Mjini (Uwanja wa Kaitaba), Nyamagana (Uwanja wa Nyamagana) na Namungo (Majaliwa Stadium).

Aidha, Halmashauri ya Wang’ing’ombe inajenga kijiji cha michezo ambacho kitakapokamilika kitakuwa na viwanja vya michezo ya soka, volleyball, Netball na Basketball .Halmashauri ya Sengerema, Mkoani Geita imeandaa ‘Concept Design’ kwa ajili ya Kituo cha Michezo,” amesema Mwinjuma.

Amesema kwa sasa Serikali ipo kwenye ukarabati mkubwa wa viwanja vya Uhuru na Benjamin Mkapa hata hivyo, Serikali inaendelea na ujenzi wa Uwanja wa Arusha (Arusha Stadium) na ukarabati viwanja vingine vitano vya mazoezi kwa ajili ya mashindano ya CHAN 2025 na AFCON 2027.

Amesema ametoa rai kwa halmashauri, wilaya na mikoa ambayo haijaguswa na miradi ya AFCON 2027 kuanza kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kujenga viwanja vya kisasa vya michezo ili pia wapate vyanzo vipya vya makusanyo katika maeneo yao.

kuzisaidia mamlaka hizo hasa zisizo na uwezo watafanya tathimini kiasi gani kinahitajika.

SOMA NA HII  RASMI: PETER BANDA NNJE YA UWANJA MPAKA MWAKANI...