Home Habari za michezo SIMBA, YANGA KUUNGANA NA WACHEZAJI WAO UGENINI

SIMBA, YANGA KUUNGANA NA WACHEZAJI WAO UGENINI

HABARI ZA SIMBA NA YANGA

Katika kuhakikisha nyota wake wanaozitumikia timu za taifa wanaziwahi mechi zao za ugenini za mashindano ya klabu Afrika wiki ijayo, Yanga na Simba zimepanga utaratibu wa wachezaji hao wanaungana na vikosi vyao moja kwa moja wakitokea katika majukumu ya timu zao za taifa na sio kuondoka nao pamoja kutokea hapa Dar es Salaam.

Mechi za mwisho za timu za taifa kucheza raundi ya pili ya hatua ya makundi ya kuwania kufuzu Afcon zitachezwa leo Jumanne, Siku tatu baada ya mechi hizo za raundi ya pili ya kuwania kufuzu Afcon, Simba itakuwa ugenini huko Libya siku moja baadaye, Yanga itakuwa ugenini dhidi ya CBE ya Ethiopia.

Ili kuwapuesha wachezaji wao na uchovu wa safari na kutumia muda mrefu angani, Simba na Yanga zimefiklia uamuzi wa kuungana na wachezaji hao katika nchi ambazo zitaenda kucheza kama ilivyothibitisha na mameneja wa timu hizo.

SOMA NA HII  FADLU AJIPANGA KIVINGINE KUIKABILI YANGA...AWAPA WACHEZAJI MAAGIZO MAALUM