Home Habari za Yanga Leo WANAYANGA MJIANDAE KWA SAPRIZI…UPEPO KUBADILIKA

WANAYANGA MJIANDAE KWA SAPRIZI…UPEPO KUBADILIKA

habari za yanga-NABI

KAMA wewe ni shabiki wa Yanga ambaye popote ilipo timu hiyo nawe unakuwepo, basi anza kujipanga mapema kwani kuna mabadiliko ambayo yataifanya klabu hiyo kuendana na baraka za Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kuelekea mchezo wa mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CBE ya Ethiopia.

Yanga ni moja kati ya timu mbili za Tanzania zilizosalia katika michuano ya CAF ikitinga raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuing’oa Vital’O ya Burundi kwa ushindi wa jumla wa mabao 10-0 na sasa imepangwa kucheza na CBE ili kusaka tiketi ya kutinga makundi. Timu nyingine ni Simba iliyoanzia hatua hiyo katika Kombe la Shirikisho Afrika ikipangwa kucheza na Al Ahli Tripoli ya Libya.

Mabadiliko ambayo huenda yakafanyika ni uwanja utakaotumika kwenye mchezo wa mkondo wa pili dhidi ya CBE ya Ethiopia.

Inaelezwa kwamba Klabu y Yanga walipanga kuupeleka mchezo huo Zanzibar katika uwanja wa New Amaan Complex, lakini kwa mujibu wa CAF uwanja huo haupo kwenye orodha ya viwanja vinavyotakiwa kutumika kwenye mechi za mkondo wa pili.

Lakini kwa taarifa zilizopo ni kwamba, Uongozi wa Yanga bado unapambana kufanikisha ombi lao la kutumia uwanja wa New Amaan Complex, ili kuwapelekea furaha mashabiki zao wa Zanzibar.

SOMA NA HII  ACHANA NA STORI ZA VIJIWENI...HUU HAPA UKWELI WA KWANINI KAMBOLE HATACHEZA MECHI YA LEO DHIDI YA SIMBA...