Home Habari za michezo WYDAD NA MZIZE MPAKA KIELEWEKE….WATUMA OFA YA ‘KUIBEBA’ NA YANGA MAZIMA….

WYDAD NA MZIZE MPAKA KIELEWEKE….WATUMA OFA YA ‘KUIBEBA’ NA YANGA MAZIMA….

HABARI ZA YANGA-MZIZE

Klabu ya Wydad Athletic imetuma ofa ya tatu kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Yanga Clement Mzize, imefahamika.

Matajiri hao kutoka ligi kuu ya Morocco wameongeza dau la usajili kufikia takribani Tsh 1.4B ambapo dau hilo linaweza kuongezeka hadi kufikia Tsh 2.1B kutegemea na makubaliano ya ziada.

Aidha klabu hiyo imeipa Yanga ofa ya kufanya pre-season ya msimu ujao Morocco ambapo Wydad watagharamikia kila kitu.

Kulingana na vyombo vya habari Morocco, wanaamini ofa hiyo ni kubwa na uongozi wa Yanga utamruhusu Mzize kwenda kujiunga na timu hiyo inayonolewa na Rulani Mokoena aliyewahi kuinoa Mamelodi Sundowns.

Yanga imeweka msimamo wa kutomuuza mchezaji huyo chini ya dau lisilopungua Tsh Bilioni 2.7.

SOMA NA HII  MENEJA WA KIBU AMKANA HADHARANI