Home Habari za michezo TFF YAIPA SIMBA NA YANGA MAELEKEZO HAYA

TFF YAIPA SIMBA NA YANGA MAELEKEZO HAYA

HABARI ZA SIMBA NA YANGA

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Wallace Karia, amezitaka timu za Ligi Kuu zenye wachezaji walio chini ya miaka 20 na hawapati nafasi za kucheza dakika nyingi, watolewe kwa mkopo kwenye timu zingine zenye mahitaji.

Rais huyo alisema hayo baada ya kumalizika kwa michuano ya Afrika Mashariki na Kati, Ukanda wa CECAFA, ikishuhudiwa Timu ya Taifa ya Tanzania, Ngorongoro Heroes, ikitwaa ubingwa kwa kuifunga Kenya mabao 2-1, katika mchezo wa fainali uliochezwa juzi, Uwanja wa KMC, Mwenge, Dar es Salaam.

Mabao ya washindi yalifungwa na Valentino Mashaka ambaye ni straika wa Simba, na Shekhan Khamisi anayeitumikia Yanga katika nafasi ya kiungo, wote wakiwa hawapati nafasi mara kwa mara katika vikosi vya kwanza vya timu hizo.

Karia alisema wachezaji hao vijana wanapaswa kupata dakika nyingi za kucheza ili wawe bora, wainue viwango vyao na kuwa na utayari kimwili.

“Tunaendelea kuzitunza timu zote za taifa chini ya miaka 17 na 20, na wale wachezaji ambao wapo kwenye timu mbalimbali za Ligi Kuu ambao hawapati nafasi kwenye vikosi vyao, klabu ziwapeleke kwa mkopo kwani zipo ambazo zinahitaji wachezaji, Ligi Kuu na hata Championship,” alisema Karia.

Akizungumzia mashindano hayo alisema yalikuwa mazuri na magumu, huku akisifu maandalizi yaliyofanyika.

“Ilikuwa ni michezo mizuri, lakini migumu, Watanzania wamepata burudani pia malengo ya CECAFA yamefikiwa kwa kuandaa na kumaliza salama washindi wakipatikana, sisi kama Watanzania tujipongeze kwa timu yetu kupata nafasi ya kucheza fainali za AFCON kwa vijana 2024/25 na pia kuwa mabingwa.

”tumerudia historia miaka minne iliyopita nchini Uganda, tulipowafunga Kenya bao 1-0 tukawa mabingwa, nakumbuka wakati huo nahodha alikuwa Dickson Job, Novatus Dismas, Abdul Selemani Sopu na wengineo,” alisema rais huyo wa TFF.

SOMA NA HII  BREAKING NEWS: BARBARA ARUDI SIMBA...MO HATAKI MASIHARA

1 COMMENT

  1. […] ya Simba SC wakiwa uwanja wa Sokoine Mbeya wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons […]

Comments are closed.