Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA FEI TOTO KUTUA SIMBA DIRISHA DOGO…TRY AGAIN AKOLEZA MOTO….

KUHUSU ISHU YA FEI TOTO KUTUA SIMBA DIRISHA DOGO…TRY AGAIN AKOLEZA MOTO….

Habari za Simba leo

MJUMBE wa bodi ya wakurugezi ya Simba, Salim Abdallah `Try Again, amesema walivyojipanga msimu wa 2024/25 wanauwezo wa kumsajili mchezaji yoyote wanayemtaka ndani na nje ya Afrika kulingana na mapendekezo ya benchi la ufundi.

Kauli hiyo ni baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa Simba kuwa wapo kwenye mchakato wa mazungumzo na kiungo wa Azam FC, Feisal Salum `Fei Toto`, kipindi cha usajili wa dirisha dogo lilalotarajiwa kufunguliwa desemba ambaye inadaiwa mkataba wake unafikia ukingoni na tayari klabu yake hiyo imeanza mazungumzo ya kumuongezea.

Try Again amesema wanafanya usajili kulingana na mahitaji ya benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Fadlu Davids, akipendekeza usajili wa kiungo huyo, itafanyika hilo.

Amesema kwa hawajafikiria suala la usajili kwa sababu bado hawajapokea mapendekezo kutoka benchi la ufundi, endapo akihitaji ya Fei Toto hawashindwa kumsajili kwa sababu wanauwezo wa kusajili mchezaji yoyote.

“Kama Kocha Fadlu anamtaka Fei Toto basi Simba haisiti kumsajili tunaenda kukutana na klabu yake kukaa meza moja kwa ajili ya mazungumzo ya biashara hakuna kinachoshindikana, sio yeye hata mchezaji yoyote yule. Hakuna mtu aliyetegemea tutamsajili Mpanzu (Elie) kwa sababu usajili wa nyota huyo ulitusumbua na kumaliza soli ya viatu.

Tulipambana sana safari za DR Congo na mataifa mengine ya Ulaya kwenda kwa ajili ya kuonana na wanaomsimamia kwa ajili ya kupata saini yake, usajili uliweza kututesa sana lakini Mwekezaji na Rais wa Simba, Mohammed Dewji alipambana na kutumia fedha kufanikiwa kumsajili,” amesema Try Again.

Ameeleza kuwa anafurahi kuona mchezaji kuamua kuchagua kuchezea Simba licha ya klabu mbalimbali kutoka mataifa mengine ikiwemo Tanzania kumtaka mchezaji huyo.

Kuhusu ushirikiano wa viongozi wa Simba ndani ya Bosi hiyo, Try amesema hakuna tofauti yoyote kati ya viongozi wa bodi na wale waliochaguliwa na wanachama kwa kuwa wanashauriana na kushirikiana na kila jambo.

“Ni kweli makundi ya hatua ya makundi ya Shirikisho Afrika yanapangwa leo (Septemba 7), tunakuwa makini yule tunayepangwa naye tunamfatilia kwa undani kufanikisha ndoto za wanasimba, Mo Dewji zinafanikiwa kwa kucheza nusu na fainali ya Shirikisho Afrika,” amesema Mjumbe huyo wa bodi.

SOMA NA HII  ODDS KUBWA GEMU ZA UCL NA EFL KUTOKA MERIDIANBET KUELEKEA WIKENDI...!