Home Habari za michezo SIMBA HII NI BALAA NA NUSU…BAJETI YA BIL 28 YAWEKWA MEZANI….MO ATIA...

SIMBA HII NI BALAA NA NUSU…BAJETI YA BIL 28 YAWEKWA MEZANI….MO ATIA MKONO WA BIL 7…

Simba SC

KLABU ya Simb imetangaza bajeti ya sh 28.6 billion kwa msimu wa 2024-2025 ikiwa ni ongezeko la sh. 3 billion kutoka bajeti ya msimu uliopita ilikuwa ni sh. 25 billion.

Hayo yamesemwa katika mkutano mkuu wa mwaka 2024 wa klabu hiyo uliofanyika katika kituo cha kimataifa cha mkutano cha Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Mhasibu wa Simba, Selemani Kahumbu amesema bajeti hiyo ya msimu huu imetegemea zaidi ya vyanzo mbalimbali vya mapato kama vile udhamini na viingilio.

“Bajeti Kuu ya msimu wa 2024/25 ni bill 28.6 kati ya hizo Rais na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohammed Dewji (Mo Dewji), ametoa billion 7, matumizi ni bill. 28. 4 na baki ni Million 200,” amesema Kahumbu.

Rais wa Simba, Mo Dew amesema leo (jana) ni siku ya heshima kubwa kuangalia maendeleo ya timu yao katika safari yao ya maendeleo ndani ya klabu hiyo.

“Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kutufikisha wote hapa na kwa niaba ya Wanasimba wote naomba kumpongeza Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu kwa uongozi wake bora na mchango wake mkubwa wa kuendeleza michezo nchini.

Hii ni safari ya pamoja na kwa pamoja tutafanikisha maono makubwa. Katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita Simba imepata mabadiliko makubwa ambayo yanalemga kuimarisha klabu yetu,” amesema Mo Dewji

Ameongeza kuwa Kujenga upya Simba kumekuwa na gharama kubwa lakini ni hatua muhimu sana, wameweza kusajili wachezaji 14 na Mpanzu (Elie) ameletwa, hatua muhimu katika kujenga kikosi imara ambacho kitaweza kushindana katika ngazi ya juu.

“Tumepata kocha mpya, Fadlu Davids pamoja na benchi mpya la ufundi, kuimarisha miundombinu sahihi ni muhimu katika kufanikisha maono yetu. Tunaendelea kubuni mifumo mipya, bodi imara na kwa pamoja tutahakikisha kila hatua inachukuliwa kwa umuhimu sana,” amesema Mo Dewji.

Ameeleza kuwa kuna ramani mpya ya Mo Simba Arena, Mradi mkubwa ambao utaweka msingi wa mafanikio yetu baadae, wanatarajia kujenga kambi bora ya mazoezi itakuwa na gym, majengo ya malazi, kituo cha lishe, bwala la kuogolea, kituo cha burudani, viwanja vitano vya kisasa, kujenga makumbusho ya klabu na kuanzisha chuo cha maendeleo ya vijana ili kulea vipaji vya soka nchini.

“Ili kufanikisha yote haya tunasubiri mchakato wa mabadiliko ya Simba kukamilika, tuko katika hatua za mwisho , Ujenzi wa miundombinu hii unakuja na gharama kubwa, ngumu kuanza huu ujenzi bila mfumo kubadilika

Tukishirikiana tunaweza kujenga Simba inayoweza kushindana ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika, malengo haya sio ndoto, bali ni lengo linaloweza kufikiwa. Pamoja tunaijenga Simba ya kesho,” amesema Rais wa Simba Mo Dewji.

Ameongeza kuwa huu wakati wa kuchukua hatua kwa nguvu zaidi, wakimaliza mchakato wa mabadiliko Simba itakuwa tayari kusimama imara na kujitegemea.

“Kwa heshima kubwa naomba tuache fitna, tuache fitna tuwe kitu kimoja, usigawanyike , fitna inatoa baraka katika klabu yetu, tumshirikishe Mwenyezi Mungu, niko na Simba katika hali na mali kufikia malengo na matarajio ya wanachama wetu,” amesema Mo Dewji.

Mwakilishi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Nicholas Mihayo amewashukuru wanasimba wote kwa kuwa na mikutano yenye amani na aliwasihi wanacheza wote kusoma na kuielewa katiba ya klabu .

“Nasisitiza wanachama kuheshimu katiba ili kuondoa migogoro isiyo na ulazima, mnatakiwa kuonyesha umoja pale timu inapopata matokeo mabaya,” amesema Mihayo.

SOMA NA HII  "KELVIN JOHN HASTAHILI KUJIITA MBAPPE....KWANZA ANADHARAU NA NIDHAMU MBOVU"....