Home Habari za michezo PAMOJA NA KUTABIRIWA MABAYA…HIVI NDIVYO FEI TOTO ANAVYOWAJIBU YANGA ‘KIKATILI’…

PAMOJA NA KUTABIRIWA MABAYA…HIVI NDIVYO FEI TOTO ANAVYOWAJIBU YANGA ‘KIKATILI’…

habari za simba

KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’, anaongoza kwa kufunga na kutoa pasi nyingi za mwisho katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara inayoendelea.

Pia nyota huyo wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), anaongoza kwa kufunga mabao mengi kwa penalti.

Hadi kufikia raundi ya 13 ya Ligi Kuu Tanzania Bara, mchezaji huyo ametoa asisti tano na kuwa juu ya orodha ya wachezaji waliotoa pasi za mwisho nyingi ambazo zilizaa mabao.

Fei Toto pia anaongoza kwa kufunga mabao mengi ya penalti, akiwa amefanya hivyo mara tatu.

Kiungo huyo wa zamani wa Yanga ambaye amefunga mabao manne katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, matatu ameyafunga kwa penalti katika mchezo kati ya timu yake dhidi ya KenGold, uliochezwa, mechi iliyochezwa Oktoba 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam wenyeji wakishinda mabao 4-1, lingine ikiwa ni Novemba 23, mwaka huu, alipofunga bao pekee kwenye Uwanja huo wa Azam ikishinda 1-0 dhidi ya Kagera Sugar.

Kwa mujibu wa dawati la takwimu , wanaofuatia kwa kufunga mabao mengi ya penalti, Jean Ahoua na Leonel Ateba, ambao wote wamefunga mabao mawili ya penalti kila mmoja na Ogochukwu Morice wa Tabora United ambaye naye amepachika penalti mbili.

Ahoua alifunga katika mchezo kati ya timu yake dhidi ya Dodoma Jiji, ikishinda bao 1-0, na dhidi ya KMC, timu yake ikishinda mabao 4-0, Ateba akipachika penalti zake, katika mchezo dhidi ya Coastal Union zikitoka sare mabao 2-2 na dhidi ya Pamba Jiji, likiwa bao pekee kwenye mechi hiyo, huku Ogochukwu akifunga dhidi ya Pamba Jiji timu yake ikishinda bao 1-0 pamoja na Mashujaa, ikishinda pia bao 1-0.

Wakati Fei Toto, akiwa na ‘asisti’ tano, wachezaji Ahoua wa Simba na Salum Kihimbwa wa Fountaina Gate, wana ‘asisti’ nne kila mmoja.

Jumla ya wachezaji saba wanashika nafasi ya tatu kwa kutoa asisti nyingi, kila mmoja akitoa tatu.

Wachezaji hao ni Stephane Aziz Ki wa Yanga, Josephat Bada na Ande Koffi wa Singida Black Stars, Yacouba Songne na Heritier Makambo wa Tabora United, Salehe Masudi wa Pamba na Ismail Mgunda wa Mashujaa.

SOMA NA HII  KISA SARE YA JUZI...GAMONDI AFUNGUKA MCHEZO MBAYA WALIOANYIWA NA AL AHLY...