Home Habari za michezo KOCHA MPYA YANGA AMRUDISHA ‘MGANGA’ WA GAMONDI…LEO NI ‘GUSA ACHIA PRO MAX’…

KOCHA MPYA YANGA AMRUDISHA ‘MGANGA’ WA GAMONDI…LEO NI ‘GUSA ACHIA PRO MAX’…

Habari za Yanga leo

KIKOSI cha Yanga kinashuka uwanjani leo kukabiliana na JKT Tanzania, lakini mashabiki wa timu hiyo watakuwa na shauku ya kujua ubora wa kocha mpya Hamdi Miloud basiĀ  jamaa ameibakisha ile falsafa ya Gusa Achia Twende Kwao kwa kuiboresha zaidi.

Gusa Achia ni falsafa alikuja nayo Sead Ramovic alipotua Yanga akitokea TS Galaxy ya Afrika Kusini ambayo katika mechi sita za Ligi ikiwa chini yake, timu hiyo ilishinda zote kwa jumla ya mabao 22 na kufungwa mawili na wakati anaondoka timu ilishinda 6-1 dhidi ya KenGold katika mechi ya saba iliyosimamiwa na wasaidizi wake, akiwamo Abdihamid Moallin.

Kocha Miloud aliyetua wiki iliyopita kuchukua nafasi ya Ramovuic aliyekimbilia CR Belouizdad ya Algeria, amesimamia mazoezi ya kwanza na kikosi hicho ndani ya siku mbili kambini Avic Town, iliyopo Kigamboni akisuka mipango michache, lakini akaibakisha staili ya uchezaji ya timu hiyo akivuta pumzi kwanza.

Katika mazoezi hayo ya siku mbili, Miloud raia wa Ufaransa alishtua kwa kusema katika maisha yake ya ukocha anataka kuona timu yake inashambulia hadi wapinzani wachanganyikiwe.

Kocha huyo ameibakisha gusa achia twende kwao, lakini akaongeza vitu vichache juu ya umakini wa kutumia nafasi huku pia akiweka msisitizo mkubwa wa eneo la ulinzi.

Hamdi alionyesha kutofurahia bao ambalo safu yake ya ulinzi ililiruhusu katika mchezo uliopita dhidi ya KenGold alilofungwa kipa Djigui Diarra na kuweka sawa hesabu zao huku akitaka umakini muda wote wa mchezo akitarajia jambo hilo.

Mfumo uleule

Miloud hajabadilisha pia mfumo wa uchezaji akiendeleza palepale walipoishia watangulizi wake akitumia mfumo wa 4-2-3-1.

Kuanzia kocha Nasreddine Nabi, Miguel Gamondi na hata Ramovic walikuwa wakitumia mfumo huo wa kisasa unaotumiwa na timu nyingi duniani.

Hatua hiyo haitawapa kazi ngumu wachezaji wa Yanga kuendeleza makali yao kama ambavyo ilikuwa kwa makocha waliopita.

Amrudisha fundi wa Gamondi

Mbadiliko ya kwanza ambayo Miloud ameyafanya ni kumrudisha kocha wa viungo aliyekuja wakati wa utawala wa Gamondi, Taibi Lagrouni.

Lagrouni aliwekwa kando Yanga wakati alipotua Ramovic kufuatia wawili hao kutofautina na sasa badaa ya Miloud kufika akamrudisha kundini.

Yanga haikumuondoa Lagrouni raia wa Morocco moja kwa moja baada ya wawili hao kutofautiana, ilichofanya uongozi wa timu hiyo ulimpa majukumu hayo hayo kwenye vikosi vyake vya wanawake na vile vya vijana.

Kurejea kwa Lagrouni ambaye ndiye alikuwa injini ya mafanikio kwa Gamondi kumemtupa nje mzungu Adnan Behlulovic ambaye tayari ameshawaaga wenzake ndani ya timu hiyo.

SOMA NA HII  DILI LA BEKI 'KIFARU' KUTUA SIMBA LAFIKIA PATAMU...KIFAA KINGINE KIPYA HIKI HAPA...NI KIBERENGE HASWA...