Home Habari za michezo KISA NDOA NA MOBETTO…? HIZI HAPA SABABU ZA AZIZ KI KUPIGWA CHINI...

KISA NDOA NA MOBETTO…? HIZI HAPA SABABU ZA AZIZ KI KUPIGWA CHINI TIMU YAKE YA TAIFA…

Habari za Yanga leo

KIUNGO mshambuliaji nyota wa Yanga, Stephane Aziz KI na beki wa kushoto wa Simba, Valentin Nouma, wametemwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Burkina Faso kinachojiandaa kwa mechi mbili za kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 na kocha wa timu hiyo ameeleza sababu.

Burkina Faso ipo katika Kundi A pamoja na Misri, Guinea Bissau, Sierra Leone, Ethiopia na Djibouti watakayocheza nayo Machi 21 kabla ya kuifuata Guinea Bissau siku tatu baadae na kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwa kukusanya pointi 5 kutokana na mechi nne. Misri inaongoza na pointi 10 na Guinea Bissau inafuata na alama zake sita.

Kocha wa kikosi hicho, Brama Traore amenukuliwa na gazeti la MwanaSpoti akitaja sababu ya kuwaacha mastaa hao hususani Aziz KI, ni kumtaka apandishe kiwango chake baada ya kutoka kuwa majeruhi, huku akimtaja Nouma kwa kutopata nafasi mara kwa mara kikosini Msimbazi.

Aziz ambaye huu ni msimu wake wa tatu kuichezea Yanga akitokea ASEC Mimosas, japo amelelewa Ivory Coast kiungo huyo ni raia wa Burkina Faso.

Kiungo huyo amekuwa akipata nafasi ya kucheza katika kikosi cha timu ya taifa hilo kutokana na kiwango bora, ambacho amekuwa akikionyesha tangu alipokuwa ASEC.

Kocha Traore alisema, aliongea na Aziz KI kabla ya kuita majina ya timu hiyo ya taifa na kiungo mshambuliaji huyo akamwambia alikuwa na majeraha hivi karibuni.

Alisema, licha ya Aziz kumhakikishia kuwa amepona na yuko vizuri, aliona ampatie muda zaidi, ili awe sawa kabisa na awape nafasi wengine.

“Aziz Ki ni mchezaji anayejua nafasi yake na yuko tayari kujitoa hata kama ni ngumu kwake, ndio maana nikaamua kumuacha apone kabisa,” alisema Traore na kuongeza;

“Kuna wachezaji wengi, hivyo sio njema kumchukua Aziz KI akiwa ametoka kuwa majeruhi, kwangu naona sio sawa pia nawaza akijitonesha tena itakuwaje, hivyo anatakiwa kupumzika, wakati mwingine nitamtumia.”

Rekodi za Aziz KI ziko moto, huku akiwa hajawahi kukosa mchezo hata mmoja katika ligi, kwani amecheza mechi zote 22 ambazo Yanga imeshiriki mpaka sasa.

Kuhusu beki wa Simba, Valentin Nouma, alisema hajacheza kwa muda mrefu, hivyo inambidi apambane ili apate nafasi ndani ya kikosi chake cha Wekundu wa Msimbazi.

“Nouma hajacheza kwa muda mrefu, anatakiwa apambane katika kikosi chake ili aweze kurudi katika timu ya Taifa.”

Hivi karibuni, ligi zitasimama ili kupisha ratiba ya FIFA.

SOMA NA HII  FT: SIMBA 1-0 JAMHURI.....BALEKE KAMA YUPO HAYUPO HIVI...KIUNGO MPYA AKIWASHA ..ILA MHH..