Home Habari za michezo KWA YANGA HII HAMDI HUMWAMBII KITU HUKO YANGA….HII HAPA ‘MIPLANI’ YAKE YA...

KWA YANGA HII HAMDI HUMWAMBII KITU HUKO YANGA….HII HAPA ‘MIPLANI’ YAKE YA ‘KUUA’..

Habari za Yanga leo

KOCHA Mkuu wa Yanga, Hamdi Miloud, amepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na wachezaji wake kuhakikisha wanapata matokeo mazuri uwanjani, akisisitiza kuwa hali hiyo inapaswa kuendelea kutokana na ushindani mkali uliopo kwenye Ligi Kuu Tanzania.

Miloud, ambaye alitwaa tuzo ya Kocha Bora wa Februari, aliongoza Yanga katika mechi tano ndani ya mwezi huo, ambapo walishinda michezo minne na kutoka sare moja dhidi ya JKT Tanzania (0-0).

Katika michezo hiyo, safu ya ushambuliaji ya Yanga ilifunga mabao 16, huku safu ya ulinzi ikiruhusu mabao mawili pekee, kwenye ligi inayoshikilia nafasi ya nne kwa ubora barani Afrika.

Akizungumza kuhusu mwenendo wa timu, Miloud alisema:”Kila mchezo tunacheza una ushindani mkubwa, na wachezaji wanajituma kuhakikisha tunapata matokeo mazuri. Tunaamini tutaendelea kuwa katika ushindani kwenye mechi zijazo.”

Kocha huyo pia alibainisha kuwa licha ya kuwapa wachezaji wake waliokosa majukumu ya timu za taifa mapumziko mafupi, amewapatia programu maalum za mazoezi ili kuhakikisha wanakuwa katika hali nzuri ya kimwili wanaporejea kambini.

Kwa sasa, Yanga inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 58 baada ya kucheza mechi 22. Safu yao ya ushambuliaji, inayoongozwa na Stephane Aziz Ki, Dube, na Clement Mzize, kila mmoja ana mabao 10.

SOMA NA HII  KISA KUGOMBEA URAIS JANGWANI...SALEH JEMBE AMLIPUA INJINIA HERSI...ADAI KAZI YA UONGOZI YANGA HAINA MSHAHARA...