Azam FC dhidi ya Simba SC
Azam FC

Azam FC vs Simba SC: Popat Afunguka Vita ya Chamazi | Ligi Kuu

Vardo September 15, 2026 7:07 pm

Makamu wa Rais wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’, ameweka wazi kuwa ingawa Simba SC ni timu kubwa na imeonyesha kiwango cha juu msimu huu, kikosi chao kipo tayari kwa mapambano na kina lengo moja tu: kupata matokeo chanya katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Azam FC watakuwa wenyeji wa Simba SC katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, kwenye mchezo unaotajiwa kuvuta hisia za mashabiki wengi kutokana na ubora na ushindani wa vikosi vyote viwili.

Ubora wa Simba na Maandalizi ya Azam FC

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Popat alikiri kuwa Simba imekuwa na muendelezo mzuri tangu msimu uliopita na imeongeza nguvu zaidi kwenye kikosi chake, jambo linalofanya pambano hilo kuwa mtihani mkubwa kwao.

Tunakwenda kupambana na timu kubwa ambayo iko vizuri tangu msimu uliopita. Ushindani wao umeongezeka na msimu huu wameongeza tena ubora kwenye kikosi chao.

Kwa sasa wamecheza mechi zao za mwanzo za Ligi ya Mabingwa Afrika na hilo limewapa nafasi ya kuongeza ubora zaidi. Sisi kama uongozi tunakiandaa na kukihamasisha kikosi chetu, huku benchi la ufundi likiwa na kocha mkubwa anayejua namna ya kukabiliana na mechi kubwa.” — Abdulkarim Amin ‘Popat’

Uzoefu wa Wachezaji Kuamua Mchezo

Popat aliongeza kuwa Azam FC inajivunia kuwa na wachezaji wenye uzoefu mkubwa wa michezo ya presha kubwa, hasa dhidi ya Simba SC. Alisisitiza kuwa nidhamu ya mchezo na kiwango watakachoonyesho uwanjani ndivyo vitakavyoamua matokeo.

Amesema Azam haitaingia uwanjani kwa hofu ya ukubwa wa Simba, bali itatumia mbinu za benchi la ufundi, maandalizi bora na uzoefu wa wachezaji wao kupata pointi tatu muhimu nyumbani.

Msisimko Tofauti wa ‘Big Game’

Mbali na pointi tatu za mchezo, kiongozi huyo alieleza kuwa michezo mikubwa kama hii huwa na hisia tofauti na furaha yake baada ya ushindi ni kubwa zaidi ukilinganisha na mechi za kawaida.

  • Furaha ya Ushindi: “Mechi kubwa zote, ushindi wake unakuwa na furaha kubwa. Ukiangalia hata nje, timu kubwa zinapocheza na kushinda, unaona namna wachezaji wanavyofurahia na jinsi chumba cha kubadilishia nguo (dressing room) kinavyochangamka.”

  • Uchungu wa Kupoteza: “Kama uongozi ukifungwa unaumia, lakini ukishinda furaha yake ni kubwa sana. Ni vitu viwili tofauti kabisa.”

Ahmed Ally: Azam FC Sio Nyonde, Simba Lazima Tutumie Akili Chamazi Iddi Nado Aichimba Biti Simba: “Lazima Tuwapige Kesho Tukae Juu Yao”