Azam FC dhidi ya Simba
Azam FC

Iddi Nado Aichimba Biti Simba: “Lazima Tuwapige Kesho Tukae Juu Yao”

Vardo September 15, 2026 7:12 pm

MSHAMBULIAJI machachari wa Azam FC, Iddi Seleman ‘Nado’, amewatahadharisha wapinzani wao Simba SC akisisitiza kuwa wamejipanga kuchukua pointi zote tatu kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu ya NBC utakaopigwa kesho Jumatano.

Nado ameeleza kuwa mechi hiyo ina uzito mkubwa mno katika mbio za ubingwa, huku ushindi ukitarajiwa kuwapa fursa ya kuwasogelea na kuwapita walioko juu kwenye msimamo wa ligi.

“Jumatano tunayo matarajio makubwa ya kuvuna alama tatu. Mchezo ni muhimu sana kwetu kwa sababu tuko kwenye mbio za ligi,” alisema Nado.

Nyota huyo aliongeza kuwa kuifunga timu kubwa kama Simba kunawapa fursa ya kubadilisha upepo wa msimamo wa ligi kwa kuwashusha wapinzani wao hao na wao kupanda juu zaidi.

“Ukimfunga mkubwa mwenzako unamshusha kwenye nafasi yake na wewe unaweza ukapanda. Ni mechi muhimu na tunahitaji pointi tatu ili tuendelee kuwasogelea walioko juu yetu,” alisisitiza.

Hata hivyo, Nado amekiri kuwa mchezo huo utakuwa wa ushindani mkubwa kutokana na ubora wa vikosi vya timu zote mbili, lakini akabainisha kuwa malengo ya Azam FC hayajabadilika — ni ushindi pekee mbele ya Wanalambalamba na mashabiki wao.

Azam FC vs Simba SC: Popat Afunguka Vita ya Chamazi | Ligi Kuu Mngqithi Atoa Onyo Uzito Yanga: “Nafasi 20 Hazitoshi, Tunapaswa Kuwa Wajihi”