Tanzania U23 Yahitaji 3-0 Kwa Kenya, Hamad Ally Aamini Mchezo Bado Upo
Tanzania U23 ina mlima mbele yake dhidi ya Kenya, lakini Kocha Mkuu Hamad Ally anaamini bado kuna nafasi ya kubadilisha story ya raundi hii baada ya kikosi chake kufanyia kazi makosa ya mchezo wa kwanza.
Vijana hao walifungwa mabao 4-1 Septemba 28 kwenye Uwanja wa Nyayo, Nairobi. Kenya ilifunga kupitia Paul Osama dakika ya pili, Lawrence Okoth dakika ya 45, Kevin Wangaya dakika ya 50 na Kelly Madada dakika ya 75, huku Shekhan Khamis akifunga bao pekee la Tanzania kwa penalti dakika ya 54.
Hesabu Ni 3-0
Marudiano yanapigwa Dar es Salaam Oktoba 6 na Tanzania inahitaji ushindi wa kuanzia mabao 3-0 bila kuruhusu bao ili kupindua matokeo ya mchezo wa kwanza na kusonga mbele. Hiyo ndiyo hesabu inayofanya kila dakika ya maandalizi kuwa muhimu.
Hamad Ally amesema benchi la ufundi limepitia kwa kina makosa yaliyotokea Nairobi na wachezaji wenyewe wamekubali kwamba walianza vibaya, hasa kipindi cha kwanza. Sasa kazi imekuwa kuondoa makosa hayo na kuingia nyumbani na intensity tofauti.
JKT Imetoa Kipimo
Katika maandalizi ya marudiano, Tanzania U23 imecheza friendly dhidi ya JKT Tanzania na kutoka sare ya 2-2. Kwa kocha, scoreline haikuwa jambo pekee; alitaka kuona kama corrections zilizofanywa mazoezini zinaanza kuonekana kwenye mazingira ya mchezo.
Hamad amesema kipimo hicho kimewapa picha ya maeneo ambayo bado yanahitaji kazi kabla ya kukutana tena na Kenya. Wachezaji pia wameahidi kupambana na kuamini kwamba wakifuata mpango kwa asilimia 100, comeback inawezekana.
Ivory Coast Inasubiri
Mshindi wa Tanzania na Kenya atasonga mbele kukutana na Ivory Coast katika hatua inayofuata. Safari hiyo ina uzito mkubwa kwa sababu fainali za AFCON U23 2027 nchini Misri pia ni njia kuelekea Michezo ya Olimpiki ya Los Angeles 2028.
Kwa Tanzania, kabla ya kufikiria Ivory Coast kuna kazi moja tu: mabao matatu, clean sheet na dakika 90 za kutokata tamaa.
Soma Hapa: Taifa Stars Yapigwa 5-0 Na AS FAR, Gamondi Apata Tahadhari Nzito Morocco