Taifa Stars katika mchezo wa kirafiki dhidi ya AS FAR Rabat nchini Morocco Oktoba 2 2026
Taifa Stars

Taifa Stars Yapigwa 5-0 Na AS FAR, Gamondi Apata Tahadhari Nzito Morocco

admin October 3, 2026 11:01 am

Taifa Stars imepata kipigo kizito cha mabao 5-0 dhidi ya AS FAR Rabat katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Morocco, matokeo ambayo yameacha maswali mengi kuhusu namna kikosi cha Miguel Gamondi kinavyoingia kwenye mechi na jinsi kinavyosimamia presha mapema.

Mambo yalianza kwenda kombo mapema sana baada ya Mohcine Bouriga kuifungia AS FAR bao dakika ya pili. Dakika ya 15 Jalal Eddine El Khfif akaongeza la pili, kabla ya Khalid Ait Ourkane kuandika bao la tatu dakika ya 23. Ndani ya dakika 23 tu, Stars ilikuwa tayari inakimbizana na mchezo.

AS FAR ilienda mapumziko ikiwa mbele 3-0 na haikuishia hapo. El Khfif akarudi tena dakika ya 75 na kufunga bao lake la pili, kabla ya Marouane Oujdou kufunga la tano dakika ya 87 na kukamilisha usiku mgumu kwa Stars.

Tatizo Halikuwa Scoreline Pekee

Kufungwa 5-0 kwenye friendly kunaweza kuonekana kama matokeo ya kawaida ya majaribio, lakini namna mabao matatu ya kwanza yalivyopatikana ndiyo jambo litakalomsumbua zaidi Gamondi. Stars haikupata muda wa kujipanga, haikudhibiti mwanzo wa mchezo na ilishindwa kupunguza kasi ya AS FAR ilipoanza kushambulia kwa nguvu.

Hili si tatizo la mchezo mmoja pekee. Stars ilifungwa 2-0 na Guinea-Bissau, ikatoka sare ya 1-1 na Madagascar, halafu sasa imepokea 5-0. Ndani ya michezo mitatu imefungwa mabao nane na kufunga moja tu, takwimu ambazo zinahitaji majibu ya haraka kabla ya mechi zenye uzito mkubwa zaidi.

Gamondi Ana Kazi Kwenye Ulinzi

Kipigo hiki kinaonyesha wazi kwamba kocha lazima aangalie namna timu inavyoanza mechi, umbali kati ya kiungo na mabeki, pamoja na jinsi wachezaji wanavyoreact baada ya kupoteza mpira. Stars ilionekana kukosa balance mapema na AS FAR ikatumia nafasi hizo bila huruma.

Friendly ndiyo sehemu ya kugundua makosa haya kabla hayajawa ghali zaidi. Lakini kama kosa lile lile linajirudia mechi baada ya mechi, hapo linatoka kwenye category ya majaribio na kuingia kwenye alarm.

Morocco Inasubiri

Stars bado ina ratiba nyingine nchini Morocco, ikiwa na mchezo mwingine wa kirafiki Oktoba 5 mjini Tangier. Baada ya kipigo hiki, Gamondi hataangalia ushindi pekee; atataka kuona reaction, concentration na timu ambayo haianguki baada ya kuruhusu bao moja.

Kwa sababu 5-0 kwenye friendly inaweza kusameheka, lakini kama wachezaji hawatajifunza lolote kutoka kwake, ndipo matokeo hayo yanakuwa na maana mbaya zaidi.

Soma Hapa: Ratiba Mpya Taifa Stars Morocco: Klabu Rabat Kwanza, Morocco U23 Oktoba 5

Simba SC Kutoka Kambi ya SA na Hesabu za Pointi 9: Kazi Inanzia Dabi ya Kariakoo! Sakata La Mastaa Yanga Stars Lafukuta, TFF Yajibu Taarifa Za Gamondi Kuchukizwa