MKUDE AGANDA NA KITAMBAA CHA UNAHODHA DAKIKA 90
JONAS Mkude, kiungo mkabaji ndani ya Simba ambaye ana uhakika wa namba kikosi cha kwanza Oktoba 26 wakati timu yake ikipewa dozi ya bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting alivaa kitambaa cha unahodha kwa muda wa dakika 90 licha ya kuwepo kwa nahodha msaidizi Mohamed Hussein, 'Tshabalala' ndani ya kikosi cha kwanza.Licha ya nahodha mkuu wa Simba, John Bocco...
HIKI NDICHO WANACHOKITAKA
Anaandika Saleh JembaBahati MBAYA, mchezo wa soka huwa hautoi furaha ya milele kwa UPANDE mmoja.Tunaweza kujifunza msimu huu wa 2020/21 ikatusaidia kuongeza ufahamu kuhusiana na soka hata kama unaipenda vipi timu yako...Ilikuwa vigumu kuamini Yanga ingeweza kuhimili mikiki hadi mechi angalau ya saba ikiwa imeshinda sita na sare moja kwa kuwa ilibadili nusu ya kikosi na ikaanza kwa kusua.Azam...
SIMBA YAOMBA MSAMAHA BAADA YA KUCHEZESHWA PIRA GWARIDE DAKIKA 180
BAADA ya kuchezeshwa pira gwaride ndani ya dakika 180 kwa msimu wa 2020/21 kwenye Ligi Kuu Bara na kuyeyusha pointi sita ilizokuwa inasaka Klabu ya Simba imeomba msamaha kwa mashabiki wao kutokana na kupitia mapito hayo magumu.Simba ambao ni mabingwa watetezi walianza kupoteza mchezo wa kwanza Oktoba 22 kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Nelson...
SARPONG: MUDA WANGU WA KUFUNGA BONGO UMEWADIA
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mghana, Michael Sarpong, amesema kuwa anaamini wakati wake wa kufunga mabao ndani ya timu hiyo umeshafika baada ya kutambua ugumu wa ligi ya Tanzania tofauti na alipokuwa awali. Sarpong amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Rayon Sports ya Rwanda amefunga bao moja pekee, akikabiliwa na ukame mzito wa mabao“Nashukuru mambo yanabadilika kadiri muda unavyokwenda,...
BM HATAHATI KUIKOSA YANGA NOVEMBA 7
KIUNGO wa Simba, Bernard Morrison kuna hatihati akaukosa mchezo wa dabi ya Kariakoo unaotarajiwa kuchezwa Novemba 7 dhidi ya watani zao wa jadi Yanga. Kwa mujibu wa Kanuni ya 39 (5)(5.2) mchezaji yeyote atayepigana au kupiga kabla ya mchezo au baada ya mchezo kumalizika basi atafungiwa michezo isiyopungua mitatu na faini isiyopungua sh. 500,00.Pia Kanuni ya 39(6) mchezaji atayebainika kukutwa...
LIVERPOOL, MANCHESTER UNITED ZAIWINDA SAINI YA BERGMANN
BERGMANN Johannesson mwenye miaka 17 anayecheza ndani ya Klabu IFK Norrkoping amewekwa kwenye rada za mabosi wa Liverpool, Juventus na Manchester United wote wakiwania saini yake.Ripoti zinaeleza kuwa Liverpool tayari wameshatuma skauti ndani ya timu yake hiyo ili kuweza kupata taarifa zake zaidi baada ya kuvutiwa na uwezo wa kinda huyo ambaye anacheza nafasi ya kiungo.Nyota huyo anaaminika ndani ya...
SIMBA KUSHUSHA WINGA MATATA
INAELEZWA kuwa uongozi wa Simba upo katika mchakato wa kumshusha winga wa kimataifa wa Msumbiji, Pachoio Lau Há King ‘Lau King’ katika dirisha dogo la usajili msimu huu. Lau King kwa sasa anakipiga katika Klabu ya UD Songo aliyokuwa akichezea kwa mkopo kiungo Luis Miquissone, raia wa Msumbiji kabla ya kujiunga na Simba akitokea Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini. Lau King,...
MTIBWA SUGAR: AZAM FC WALIKUWA WANAKUTANA NA TIMU NDOGO
UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa kikubwa ambacho kinawabeba ndani ya uwanja ni juhudi na kujituma kwa wachezaji wao matokeo mabaya ilikuwa ni mpito kwao.Imekuwa ya kwanza kuitungua Klabu ya Azam FC kwa msimu wa 2020/21 ambayo ilicheza mechi saba bila kupoteza ambapo umeweka bayana kuwa wapinzani wao walikuwa wanakutana na timu ndongo ndio maana walikuwa wanashinda.Mtibwa Sugar inayonolewa...
AZAM FC:HAIKUWA FUNGU LETU MTIBWA SUGAR
UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar halikuwa fungu lao la kupata ndio maana wamepoteza kwa kufungwa bao 1-0.Azam FC inayofundishwa na Kocha Mkuu, Aristica Cioaba ilikuwa imecheza jumla ya mechi saba bila kupoteza ilipoteza mchezo wake wa kwanza jana, Oktoba 26, Uwanja wa Jamhuri Morogoro kwa kufungwa na Mtibwa Sugar.Bao pekee la ushindi...