AUBAMEYANG AFURAHIA MAISHA YAKE NDANI YA ARSENAL
PIERRE Emerick Aubameyang amesema kuwa bado yupo ndani ya Arseanl kwa sasa wakati wa kusepa ukifika ataweka wazi.Nyota huyo raia wa Gabon anayekipiga timu yake ya Taifa akiwa ni nahodha kwenye timu zote anazocheza ikiwa ni pamoja na Arsenal ana umri wa miaka 30.Auba amekuwa akihusishwa kusepa ndani ya klabu hiyo huku ikielezwa kuwa Barcelona ipo mlangoni kuiwinda saini...
JIPATIE NAKALA YAKO YA BETIKA BURE KABISA
Gazeti la BETIKA lipo mtaani Jumatano hii, hili ni gazeti la bure yaani haliuzwi, fika popote kwa muuzaji wa magazeti utajipatia nakala yako bila malipo.Ndani ya Betika kuna elimu kuhusu janga la Corona, jinsi ya kujikinga wakati huu ambapo dunia inapambana na virusi hivyo.Kuna habari, makala za michezo na burudani bila kusahau takwimu za michezo mbalimbali pamoja na dondoo...
MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO
MUONEKANO wa Ukurasa wa mbele Gazeti la Championi Jumatano, nafasi ya kushinda ndinga mpya ni yako
DILI LA KAGERE KUIBUKIA HISPANIA LIMEKAA HIVI
WAKALA wa straika wa Simba, Meddie Kagere, Patrick Gakumba, amefunguka kwamba dili la straika wake kutakiwa na klabu ya Hispania limekuwepo na kitu pekee ambacho kinakwamisha suala hilo ni mabosi wa mchezaji wake, Simba.Gakumba ameongezea kuwa alipata dili hilo la Kagere la kutakiwa na moja ya klabu ambazo zinashiriki Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) ambapo walikuwa wanamhitaji straika...
BARCELONA HAWAPOI, WAKIMKOSA LAUTARO BASI MBADALA WAKE NI ISAK
KLABU ya Barcelona imejipanga kufanya maamuzi magumu endapo tu itashindwa kufanikiwa kumpata staa wa Inter Milan, Lautaro Martinez basi itageukia kwa Real Sociedad kwa kumnasa Alexander Isak.Barca imekuwa ikipambana kwa bidii kwa kuhakikisha inampata Martinez lakini Inter ni kama inaonekana kama haina mpango wa kumuachia staa huyo. Klabu hiyo kwa sasa imejipanga kuona inafanikiwa kumsajili Isak ambaye anakipiga katika Klabu...
WACHEZAJI WA SIMBA WAFUNGUKA A-Z WALIVYOPOTEZA FAINAL YA CAF 1993..WAMTAJA DEWJI NA TFF
LICHA ya miaka 27 kupita, kovu la kipigo cha mabao 2-0 cha Simba dhidi ya Stella Abdijan ya Ivory Coast kwenye fainali ya CAF halijafutika kwa nyota wa Simba ambao wamefafanua tuhuma za kuuza mechi na wachezaji kuzichapa wenyewe kwa wenyewe katika vyumba vya kubadilishia nguo.Simba iliruhusu kipigo cha mabao 2-0 baada ya suluhu ugenini nchini Ivory Coast, mechi...
WAKALA – SIMBA WALIKATAA MILIONI 500 ZA SAMATTA
WAKALA wa kimataifa wa soka nchini, Ally Saleh amefichua kuwa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ana nafasi kubwa ya kubaki katika Ligi Kuu ya England hata ikitokea timu yake Aston Villa itashuka daraja.“Kuna kampuni ya uwakala ambayo nimekuwa nawasiliana nayo kwa ukaribu imenihakikishia kuwa upo uwezekano wa Samatta kununuliwa hadi kwa dau la Sh 50 bilioni (Pauni 17.3...
YANGA YA GSM NI MOTO WA KUOTEA MBALI.. VIFAA VIPYA KUTOKA CONGO NA KENYA VYANUKIA JANGWANI
KOCHA wa Yanga, Luc Aymael, amewaambia viongozi kwamba katika vitu ambavyo anataka msimu ujao ni kuona timu hiyo ikicheza mpira wa kasi na pasi nyingi.Katika ripoti yake hata kwenye mikutano kwa njia ya video ambazo wamekuwa wakifanya kila mara, amewasisitiza kwamba anataka kuisuka Yanga tofauti kabisa na iliyozoeleka machoni mwa mashabiki na anataka vikombe.Katika moja ya mapendekezo yake ni...
SIMBA WAJANJA KWELI WAMUWAHI YULE MTUPIAJI ALIYEKUWA ANAWINDWA NA YANGA
INAELEZWA kuwa Uongozi wa Simba umeamua kumalizana na mchezaji wao Deo Kanda ambaye alikuwa kwenye hesabu za kutua ndani ya Yanga msimu ujao.Kanda ambaye alitua Bongo akitokea Congo kwa mkopo wa muda wa mwaka mmoja ambapo msimu ukimeguka naye dili lake lilikuwa linameguka ameongezewa dili jingine.Habari zinaeleza kuwa kutokana na mchango wake kuwa mkubwa ameongezewa kandarasi ya miaka miwili...
AZAM COMPLEX SASA MAMBO SAFI, YAINGIA ANGA ZA TP MAZEMBE
HATIMAYE ukarabati wa Uwanja wa Azam Complex, umekamilika kwa asilimia 100.Uwanja huo ulikuwa unafanyiwa ukarabati ambapo nyasi zote zilifumuliwa na kuanza kuwekwa upya kabisa na inaelezwa kuwa zaidi ya bilioni tatu zimewekwa chini.Wakati wa maboresho Azam FC walikuwa wanatumia uwanja wa Uhuru na Taifa kwenye mechi zao za nyumbani sasa watarejea Chamazi.Iwapo Ligi Kuu Bara itarejea hivi karibuni kutokana...