BREAKING:ISHU YA CHAMA YATINGA TFF
KUTOKANA na Uongozi wa Yanga kudai kwamba umefanya mazungumzo na Clatous Chama, Simba wamekimbilia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
ALLIANCE NI KIBOKO, YACHIMBISHA JUMLAJUMLA MAKOCHA WANNE
KLABU ya Alliance School yenye maskani yake mkoani Mwanza msimu huu wa Ligi Kuu Bara imeweka rekodi ya kuwachimbisha makocha wanne kazi mazima.Ikiwa kwa sasa msimu wa 2019/20 umesimamishwa na Serikali kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona tayari makocha wanne wamepigwa chini ndani ya Alliance.Kocha wa kwanza kutimuliwa msimu huu ndani ya ligi alikuwa Athuman Bilali wengi hupenda kumuita...
NYOTA WA MTIBWA SUGAR AJICHIMBIA FUKWENI KUPIGA MATIZI
ABDULHAMAN Humud, nyota anayekipiga Mtibwa Sugar amesema kuwa anaendelea kupiga mazoezi kwenye fukwe li kulinda kipaji chake.Akizungumza na Saleh Jembe, Humud amesema kuwa kwa wakati huu wa kujikinga dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona,amekuwa akifanya mazoezi yake binafsi ili kulinda kipaji."Mimi nipo vema na ninaendelea na kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona ila ninaendelea kufanya mazoezi binafsi...
BOB HAISA AREJEA NA PENZI LA KARAHA
BOB Haisa, msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye anaimba mtindo wa mduara amesema kuwa amerejea tena kwenye fani hiyo akiwa na kigongo kipya ambacho anaamini kitamrejesha kwenye chati.Ngoma yake ya 'Nipe Mgongo' ilimpa mafanikio makubwa na kumfanya ajulikane nje na ndani ya nchi kwa sasa kigongo chake kipya kinaitwa Penzi la Karaha.Akizungumza na Saleh Jembe, Bob Haisa amesema...
NIYONZIMA: AFYA NI MUHIMU, TUCHUKUE TAHADHARI
HARUNA Niyonzima, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa ni muhimu kwa kila mmoja kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona ili kuwa salama.Kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imesimamishwa kwa muda ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.Akizungumza na Saleh Jembe, Niyonzima amesema kuwa kuna mambo mengi kwa sasa yamesimama ila ni muhimu kuzingatia afya kwanza kisha mengine yatafuata."Muhimu...
ISHU YA CHAMA, TAMKO LATOLEWA NA SIMBA, YANGA WAJIWEKA KANDO
UONGOZI wa Simba umesema kuwa hakuna timu itakayomchomoa nyota wao raia wa Zambia kwa sasa, Clatous Chama kutokana na kuhitaji huduma yake.Kumekuwa na mvutano mkubwa kwa sasa kuhusu Chama kati ya mabosi wa Simba na Yanga ambao wanaelezwa kuiwinda saini yake huku Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela akieleza kuwa wamejiweka pembeni kuhusu suala hilo.Ofisa Habari wa Simba, Haji...
MTIBWA SUGAR: MUHIMU KUCHUKUA TAHADHARI YA VIRUSI VYA CORONA
UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa kwa sasa ni wakati wa kila mmoja kuchukua tahadhari kuhusu Virusi vya Corona kuwa janga la dunia.Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kuwa kwa sasa ni jukumu la kila mmoja kuchukua tahadhari ili kujilinda na Virusi vya Corona."Ni muhimu kila mmoja kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona,...
KIKOSI CHA KWANZA CHA OFISA HABARI WA SIMBA AMTAJA MUUAJI WA SIMBA
HIKI hapa kikosi cha Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amtaja muuaji wao aliyewatungua Machi 8 Uwanja wa Taifa:-1. Manula wa Simba2.Kapombe wa Simba3.Job wa Mtibwa Sugar4. Tshabalala wa Simba5. Mwamnyeto wa Coastal Union6. Sure Boy wa Azam FC7. Tshishimbi wa Yanga8. Chama wa Simba9. Morrison wa Yanga10. Bocco wa Simba11. Kagere wa Simba
MBELGIJI WA YANGA YAMKUTA HUKO, AKWAMA KUTUA BONGO MARA MBILI
LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amekwama mara ya pili kurejea Bongo kutokana na Serikali kuzuia ndege kupaa ili kuzuia maambukizi ya Virusi vya Corona.Eymael alikwea pipa mpaka nchini kwao Ubelgiji ili akapate mapumziko mafupi pamoja na mpango wake wa kuoa baada ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.Kocha huyo awali alipanga kurejea Bongo Jumamosi...
MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA BETIKA LIPO MTAANI BURE KABISA
MUONEKANO wa Ukurasa wa mbele Gazeti la Betika, lipo mtaani jipatie nakala yako BURE kabisa