KOCHA COASTAL UNION AWATAKA WACHEZAJI KUCHUKUA TAHADHARI NA KULINDA VIPAJI VYAO PIA
JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa ni muhimu kwa wachezaji wake kufanya mazoezi kwa sasa kujiweka sawa licha ya kupitia kipindi kigumu.Ligi Kuu Tanzania Bara imesimamishwa na Serikali ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo wachezaji wapo nyumbani baada ya kambi kuvunjwa.Mgunda amesema:"Ni kipindi kigumu ambacho tunapitia kwa sasa ni dunia nzima inapambana lakini ni...
MUUAJI WA SIMBA ABADILISHIWA MAZOEZI
BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga amebadilishiwa program na kocha wake, Luc Eymael ambapo kwa sasa anafanya mazoezi ufukweni.Morrison aliwafunga Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Machi 8, Uwanja wa Taifa.Awali Morrison alikuwa akifanya mazoezi nyumbani tu katika kipindi hiki cha ligi kusimama kutokana na uwepo wa Virusi vya Corona, ambapo benchi la ufundi la Yanga liliwapa...
VITALIS MAYANGA HAELEWI KILICHOMFANYA AWE BUTU NDANI YA KMC
VITALIS Mayanga mshambuliaji anayekipiga ndani ya Ndanda FC amesema kuwa mpaka sasa haelewi kilichomkwakmisha kufunga mabao alipokuwa ndani ya Klabu ya KMC.Mayanga alipewa dili la miaka miwili ndani ya KMC mkataba wake ulivunjwa baada ya mabosi kushindwa kuelewa uwezo wake na alisepa akiwa hajafunga bao hata moja.Mayanga ambaye alipoibuka ndani ya Ndanda amekuwa akicheka na nyavu kabla ya Ligi...
GWIJI MANCHESTER UNITED AMPA TANO FERNANDES
GWIJI wa Manchester United, Paul Scholes, amesifu mchango ulioletwa na Bruno Fernandes klabuni hapo, akisema raia huyo wa Ureno amekuja na kitu kilichokosekana kwa muda mrefu United.Mara baada ya kujiunga akitokea Sportling Januari, Fernandes ameisaidia United kucheza mechi 11 mfululizo bila kupoteza kabla ya ligi kusimamishwa kutokana na Virusi vya Corona.Katika mechi tisa za michuano yote akiwa na United,...
NYOTA WA GOFU APIGA HESABU ZA KUIBUKIA KWENYE BIASHARA KUINUA KIPATO
NYOTA wa gofu Afrika Mashariki na Kati anayekipiga katika klabu ya gofu ya Lugalo jijini Dar es Salaam, Angel Eaton, amesema mipango yake hivi karibuni ni kufungua mgahawa wa chakula utakaomsaidia kuongeza kipato tofauti na anachokipata akishiriki mashindano tofauti.Eaton amesema kuwa mchezo wa gofu haumlipi kama watu wanavyodhani ndio maana anaingia kwenye ujasiriamali.“Ukiangalia nyumbani nimejaza makombe kibao lakini sina hata...
KMC WAVUNJA KAMBI, WACHEZAJI WANAFUTILIWA KWENYE MITANDAO
UONGOZI wa KMC umesema kuwa unawafuatilia wachezaji wao namna wanavyofanya mazoezi kupitia makundi ya WhatsApp jambo ambalo linawafanya wazidi kufanya mazoezi zaidi.Ligi Kuu Bara iliposimamishwa wachezaji wa KMC iliripotiwa kuwa wapo kambini na wanaendelea na mazoezi ila kwa sasa uongozi umesema kuwa umevunja kambi na kila mchezaji anaendelea na mazoezi nyumbani.Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa KMC, Anwary...
MASAU BWIRE: TUSISAHAU KUOMBA ILI HALI IWE SHWARI
MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa ni wakati wa kila mtanzania kuomba kwa Mungu ili janga la Corona lipite na maisha yaendelee.Kwa sasa dunia nzima inapambana kutafuta njia ya kutoka kwenye maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo kwenye sekta ya michezo ligi nyingi zimesimamishwa kupisha maambukizi zaidi ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu Tanzania Bara.Akizungumza na...
UONGOZI WA SIMBA WAHITAJI KUONGEZA MASHINE MBILI ZA KAZI, MAJINA YAO HAYA HAPA
UONGOZI wa Simba umesema kuwa mpango mkubwa kwenye kuboresha kikosi chao kwa sasa ni sehemu ya mshambuliaji ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho.Wakati Ligi Kuu Bara inasimamishwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona, safu ya ushambuliaji ya Simba ilikuwa inaongoza kwa kutupia mabao ambao ilikuwa imefunga mabao 63.Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa kuna ulazima wa kuongeza...
YANGA WAMEAMUA, SASA KUMVUTIA KASI KIUNGO HUYU MATATA ANAYEKIPIGA TIMU YA TAIFA
IMEELEZWA kuwa Klabu ya Yanga inaisaka saini ya nyota wa Kariobangi Sharks FC Yidah Sven Yidah ili aongeze nguvu kwenye kikosi hicho.Nyota huyo ambaye ni kiungo raia wa Kenya anakipiga pia kwenye timu ya Taifa ya chini ya miaka 23.Uwezo wake wa kukaba na kuzuia mashambulizi ya wapinzani inaelezwa kuwa sababu ya Yanga kuvutiwa naye na ikiwa mambo yatakwenda...
BRUNO TARIMO AJIPA UBALOZI NCHINI SERBIA
BRUNO Tarimo ‘Vifuaviwili’ bondia wa ngumi za kulipwa ambaye ni bingwa wa International Super Feather Weight alioupata nchini Serbia kwa pointi mbele ya bondia Scheka Gurdijeljac raia wa Serbia amesema kuwa ameamua kuwa balozi wa kupambana na Virusi vya Corona.Kwa sasa Vifuaviwili anaishi nchini Serbia ambapo anaendelea kufanya mazoezi ndani ya nyumba baada ya Serikali kuzuia watu kutoka nje...