MTIBWA SUGAR: MASHABIKI, WACHEZAJI WACHUKUE TAHADHARI YA CORONA

0

THOBIAS Kifaru, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema kuwa watanzania na mashabiki wanapaswa wachukue tahadhari ya Virusi vya Corona kwani ni janga la dunia nzima.Kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona, Serikali ilizuia mikusanyiko isiyo ya lazima ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu Bara.Mtibwa Sugar ilivunja kambi yao Machi 17 na sasa wachezaji wapo nyumbani wakiendelea na mazoezi binafsi...

AZAM FC: BADO HATUJAJUA HATMA YA LIGI ITAKUAJE

0

UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa bado haujajua hatma ya Ligi Kuu Bara kwa sasa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona.Azam ipo nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 28 kibindoni imejikusanyia pointi 54 huku kinara akiwa ni Simba mwenye pointi 71 akiwa amecheza pia mechi 28.Akizungumza na Saleh Jembe, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin amesema...

KAHEZA: BADO NAJIFUA NA KUCHUKUA TAHADHARI PIA

0

MARCEL Kaheza, mshambuliaji wa Polisi Tanzania amesema kuwa kwa sasa anaendelea na program maalumu ili kulinda kipaji chake kuwa bora.Kaheza akiwa ndani ya Polisi Tanzania ametupia mabao saba na ana pasi tano za mabao mguuni mwake.Akizungumza na Saleh Jembe, Kaheza amesema kuwa amekuwa akifanya mazoezi ili kujilinda kubaki kwenye ubora wake."Mazoezi kwangu ni muhimu na programu ambayo tumepewa ninaifuata...

KOCHA LIGI KUU AWAPA MAJUKUMU YA KUWA MABALOZI WACHEZAJI WAKE

0

JACKSON Mayanja aliyekuwa Kocha Mkuu wa KMC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara amesema kuwa kuna umuhimu wa wachezaji kuchukua tahadhari wakiwa nyumbani kipindi hiki kigumu cha kupambana na Virusi vya Corona.Akizungumza na Saleh Jembe, Mayanja ambaye kwa sasa ni Kocha Mkuu wa timu ya KFC ya Uganda inayoshiriki Ligi Kuu ya Uganda amesema afya ya kila mmoja ina umuhimu...

WACHEZAJI YANGA WAPIGWA STOP KULA CHIPSI

0

JUMA Abdul, nahodha msaidizi wa Yanga amesema kuwa wachezaji wameshauriwa kuacha kula vyakula vyenye mafuta mengi ili kuepuka kuongezeka uzito ghafla.Kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo ni janga la dunia.Akizungumza na Saleh Jembe, Abdul amesema kuwa kila mchezaji amepewa program yake ya kuifanya na ushauri wa kufuata akiwa nyumbani."Kuna program ambayo...

KOCHA SIMBA: WACHEZAJI WASIOFANYA MAZOEZI WANAZIFELISHA TIMU

0

SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa kwa kipindi hiki kigumu cha maambukizi ya Virusi vya Corona wachezaji ambao hawatafuata program walizopewa watarudisha nyuma maendeleo ya timu.Kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imesimamishwa ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa ni  jambo la msingi kwa wachezaji wote kuzingatia program ambazo wamepewa na...

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE WA GAZETI LA SPOTIXTRA LIPO MTAANI

0

MUONEKANO wa Ukurasa wa mbele Gazeti la SpotiXtra Jumapili, nafasi ya kushinda kwa jero tu ni yako

YANGA YAMVUTIA KASI NYOTA ANAYEKIPIGA NDANI YA CONGO, MAMBO NI MOTO

0

INAELEZWA kuwa bosi mmoja wa GSM anatarajiwa kupanda ndege hadi nchini DR Congo kwenda kumalizana na winga wa AS Vita, Tuisila Kisinda mwenye miaka 20 akimudu kucheza kiungo wa pembeni (winga). Winga huyo inaelezwa aliwahi kuwaniwa na Simba, Desemba, mwaka jana lakini dili halikufanikiwa.Taarifa za uhakika zinasema kuwa Kisinda anakuja Yanga kufuatia mapendekezo ya kocha Luc Eymael, ambaye aliagiza kusajiliwa...

ISHU YA BEKI WA COASTAL UNION KUIBUKIA SIMBA IPO NAMNA HII

0

BAKARI Mwamnyeto, nahodha wa Coastal Union amesema kuwa hana hiyana iwapo kikosi cha Simba kitahitaji saini yake. Inaelezwa kuwa mabosi wa Simba wanahitaji huduma ya  beki huyo hali iliyofanya kumtengea dau la milioni 85.Safu yake ya ulinzi imejijengea ukuta makini ambapo inashika nafasi ya pili kwa kuruhusu mabao machache ikiwa imefungwa 19 msimu huu na kinara akiwa ni Simba ambaye...